WAZIRI wa Viwanda na Biashara Prof Kitila Mkumbo amewataka Wakuu wa Taasisi zilizo chini ya Wizara hiyo kufanya kazi kwa mujibu wa Sheria, Kanuni na Taratibu zinazotumika kusimamia taasisi hizo na sikuwa kikwazo katika kutoa huduma bora kwa wananchi.
Waziri Mkumbo aliyasema hayo alipokuwa akitoa mwelekeo wa utekelezaji wa majukumu ya Wizara katika kikao na Wakuu wa Taasisi hizo kilichofanyika tarehe 09/04/2021 katika ukumbi wa Chuo cha Biashara jijini Dodoma.
“Taasisi zote zilizochini ya Wizara ya Viwanda zinamchango mkubwa katika utekelezaji wa majukumu ya Wizara hivyo nawasihi muendelee kufanya kazi kwa mujibu wa Sheria Kanuni na taratibu zinazosimamia taasisi zenu katika utoaji wa huduma bora kwa wananchi na si kuwa kikwazo” Amesema Waziri Mkumbo.
Aidha, Wakuu wa Taasisi waliohudhuria kikao hicho kutoka TBS, WMA, BRELA, TANTRADE, SIDO, NDC, EPZA, FCC, FCT, WRRB, TIRDO, CAMARTEC, TEMDO na CBE walipata fursa ya kutoa maoni na changamoto mbalimbali zinazozikabili taasisi hizo katika utekelezaji wa majukumu yake kwa Waziri wa Viwanda na Biashara.
Waziri Mkumbo ameahidi kuendelea kupokea ushauri wa kitaalamu kutoka katika taasisi hizo pamoja na kutatua changamoto mbalimbali zinazozikabili taasisi hizo katika utekelezaji wa majukumu yake ikiwemo upatikanaji Bodi zinazofanya kazi katika kila taasisi ili kurahisisha utoaji wa maamuzi sahihi na kwa wakati.
Naye Naibu Waziri akiongea na Wakuu wa Taasisi hizo, alisema kuwa mchango wa taasisi hizo ni muhimu na zinategemewa katika kuifanikisha Wizara kufikia malengo ya taifa katika ukuaji wa viwanda na biashara shindani na hivyo kukuza uchumi wa nchi.
Waziri wa Viwanda na Biashara
Prof. Kitila Mkumbo (Mb) akitoa mwelekeo wa utekelezaji wa majukumu ya
Wizara alipokutana na Wakuu wa Taasisi zilizopo chini ya Wizara katika
kikao kilichofanyika tarehe 09/04/2021 katika ukumbi wa Chuo cha
Biashara jijini Dodoma.
Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Ushindani Dkt John Mduma akitoa maoni kuhusu ukamilishaji wa mapitio mbalimbali ya Sera na Sheria zinazosimamia taasisi zilizopo chini ya Wizara ili kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi kwa Mhe. Waziri wa Viwanda na Biashara Prof. Kitila Mkumbo katika kikao na wakuu wa taasisi hizo kilichofanyika tarehe 09/04/2021 katika ukumbi wa Chuo cha Biashara jijini Dodoma.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo (SIDO) Mhandisi Prof. Sylvester Mpanduji akitoa maoni kuhusu uboreshaji wa huduma zinazotolewa na SIDO kwa Mhe. Waziri wa Viwanda na Biashara Prof. Kitila Mkumbo katika kikao na Wakuu wa Taasisi zilizopo chini ya Wizara kilichofanyika tarehe 09/04/2021 katika ukumbi wa Chuo cha Biashara jijini Dodoma.
Katibu Mkuu wa Naibu Waziri wa
Viwanda na Biashara Bw. Dotto James akifafanua jambo katika Kikao cha
Wizara na Wakuu wa Taasisi zake Kikao hicho kilicholenga kujadili
mwelekeo wa utekelezaji wa majukumu ya Wizara kilifanyika tarehe
09/04/2021 katika ukumbi wa Chuo cha Biashara jijini Dodoma.
Waziri wa Viwanda na Biashara
Prof. Kitila Mkumbo (Mb) akitoa mwelekeo wa utekelezaji wa majukumu ya
Wizara alipokutana na Wakuu wa Taasisi zilizopo chini ya Wizara katika
kikao kilichofanyika tarehe 09/04/2021 katika ukumbi wa Chuo cha
Biashara jijini Dodoma.
Kushoto ni Kaimu Afisa
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Vipimo (WMA) Bi. Stella Kahwa, Katikati ni
Mrajis wa Baraza la Ushindani Bw Renatus Rutatinisiwa akifuatiwa na
Kaimu Mkurugenzi Mkuu waa NDC Bi Rhobi Sattima wasilikiliza maelekezo
ya Waziri wa Viwanda na Biashara Prof. Kitila Mkumbo katika kikao na
Wakuu wa Taasisi zilizopo chini ya Wizara kilichofanyika tarehe
09/04/2021 katika ukumbi wa Chuo cha Biashara jijini Dodoma.
Naibu Waziri wa Viwanda na
Biashara Mhe. Exaud Kigahe (Mb) (kulia) akiwa na Naibu Katibu Mkuu wa
Wizara ya Viwanda na Biashara Dkt Hashil Abdallah (kushoto) wakiwa
katika Kikao cha Wizara na Wakuu wa Taasisi zake. Kikao hicho
kilicholenga kujadili mwelekeo wa utekelezaji wa majukumu ya Wizara
kilifanyika tarehe 09/04/2021 katika ukumbi wa Chuo cha Biashara
jijini Dodoma
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...