Na Abdullatif Yunus Michuzi TV.
Serikali tayari imetenga Milioni 579 za Ujenzi wa Daraja na ukarabati wa Barabara Eneo Korofi la Katokoro Kata Katoro Halmashauri ya Wilaya Bukoba, kazi inayotegemewa kuanza Mwezi Aprili Mwaka huu.
Akiongea na Wananchi wa Kata Katoro wakati akijibu Risala iliyosomwa kwake Mbunge wa Jimbo la Bukoba Vijijini Dkt Samson Rweikiza, katika Mkutano wa Hadhara alipofika Kata hiyo kufahamu changamoto zilizopo na kuwashukuru kwa kumpatia Kura katika Uchaguzi uliopita.
Katika shukrani hizo Dkt Rweikiza (MB) hakusita kuwakumbusha Wananchi hao Juu ya Miradi iliyotekelezwa kwa kipindi cha Miaka mitano iliyopita licha ya Kata hiyo kuongozwa na upinzani, ikiwemo Miradi ya Afya, Elimu, Umeme, Barabara ambayo imetekelezwa na CCM bila hiyana.
"... Tukiwa kwenye Kampeini mengi tuliyasema na kuyaahidi, ingawa wengine walidhani Ni Uongo lakini Mimi sipendi kusema Uongo, na leo Nimekuja kutekeleza ahadi yangu.." Alisema Dkt Rweikiza (Mb).
Ameongeza kuwaomba Wanachi wa Kata hiyo kuendelea kujitolea Nguvu zao kuchangia maendeleo huku akichangia Milioni Tano Kati ya Milioni Sita alizoahidi kuchangia.
Aidha kuhusu Mradi wa Maji amewaomba Wananchi kuendelea kuwa wavumilivu wakati ambapo Serikali inaendelea na Tatatibu za usanifu na uhakiki wa Mradi Mkubwa wa Maji kwa Kata Sita za Bukoba Vijijini zikiwemo kata za Izimbya, Mugajwale, Ruhunga, Katoro, Kaibanja na Kyaitoke.
Baadhi ya Mitumbwi ikiwa imeegeshwa kusubiri kuvusha Wananchi eneo la Katokoro Kata Katoro Bukoba Vijijini, Usafiri huo ukiwa Ni msaada Mkubwa kwa Wananchi wa maeneo hayo kwa Sasa.
Dkt. Samson Rweikiza (Mb) akiongea katika Mkutano wa Hadhara alipofika Kata Katoro Bukoba Vijijini, ili kubaini Changamoto zilizopo Kata hiyo pamoja na kuwashukuru kwa kumchagua yeye na Chama Cha Mapinduzi Uchaguzi Mkuu uliopita.
Wananchi wa Jimbo la Bukoba Vijijini kutoka Kata Katoro na Viunga vyake wakiendelea kumsikiliza Mbunge wao Dkt Rweikiza alipofika kuwashukuru mapama Aprili 09 Mwaka huu.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...