Nteghenjwa Hosseah, Tanga.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Ummy
Mwalimu amesema atazifumua Sekretariet za Mikoa endapo hazitatekeleza
majukumu yake ipasavyo.
Waziri Ummy ameyasema
hayo alipokua akizungumza na Sekretariet ya Mkoa wa Tanga mapema tarehe
26.04.2021 katika Ukumbi wa Ofiso ya Mkuu wa Mkoa Mkpani hapo.
Mhe.Ummy
amesema jicho langu la karibu ni Sekretarieti za Mikoa sitaki nianze
kupambana na Halmashauri 184 wakati nina watu kwenye Sekretarieti za
Mikoa ambao wako karibu kimazingira na kiutendaji na halmashauri hizo
ninataka watekeleze majukumu yao ipasavyo na mimi nipate taarifa zote
kutoka kwao.
‘Sitaki kuona Sekretarieti za
Mikoa ni watu wa ‘kucompile’ taarifa za Halmashauri tu ninataka kuona
zinakaa na Halmashauri zao zinawashauri, mnaweka mambo sawa na
mnazisimamia ipasavyo katika utekelezaji wa majuku yako ya kila siku’
Aidha
aliongeza kuwa ‘Sekretariet ya Mkoa ambayo nitaibani kuwa wataalam wake
ni wazembe na hawatekelezi majukumu yao ipasavyo itabidi watupishe
tuweke watu watakaochapa kazi kwa weledi na umakini wa hali ya juu huku
wakienda na muda.
Mwisho Waziri Ummy amezitaka
Sekratariet za Mikoa kusimamia ukusanyaji wa Mapato ya Halmashauri
zilizoko kwenye Mikoa yao, Matumizi ya Fedha za mapato ya ndani ikiwa ni
pamoja na kupeleka fedha hizo kwenye miradi ya maendeleo na utoaji wa
mikopo ya asilimia kumi huku wakisimamia marejesho ya mikopo hiyo ili
izunguke kwa wananchi wengine wafaidike na mikopo hiyo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...