Na Mwandishi wetu, Babati
MWENDESHA
mashtaka wa Mkoa wa Manyara, Mutalemwa Kishenyi anashikiliwa na Taasisi
ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa TAKUKURU Mkoa wa Manyara, kwa tuhuma
za kuomba na kupokea rushwa ya shilingi milioni tano.
Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Manyara, Holle Joseph Makungu ameyasema hayo Mjini Babati wakati akizungumza Aprili 25, mwaka huu.
Makungu
amesema kwamba Mwendesha mashtaka huyo wa Mkoa wa Manyara, wakili
Kishenyi amekamatwa Aprili 23 mjini Babati usiku akiwa anapokea kiasi
cha shilingi milioni tano kwa watuhumiwa wa makosa ya jinai.
Amesema
watuhumiwa hao walikamatwa katika upekuzi uliofanywa na mamlaka za
dola ambapo walikamatwa na risasi 370 na stika bandia zenye thamani ya
shilingi bilioni sita.
Mkuu huyo wa TAKUKURU amesema kuwa Mwendesha mashtaka huyo alikamatwa wakati akipokea rushwa ili kuwasaidia watuhumiwa hao.
"Uchunguzi
zaidi wa tuhuma hizi unaendelea na ukikamilika mtuhumiwa huyu
atafikishwa mahakamani ili kujibu tuhuma husika," amesema Makungu.
Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Manyara, Holle Joseph Makungu akizungumza na waandishi wa habari Mjini Babati.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...