Na Pamela Mollel,Arusha

Mkurugenzi wa jiji la Arusha Dkt. John Pima amevialika vikundi vya wanafunzi kutoka chuo cha uhasibu Arusha (IAA) kwenda kupata mkopo ili wajiendeleze.

Akizungumza wakati wa siku ya kutambua vipaji na bunifu mbalimbali za wanafunzi ili kuviendeleza maarufu kama "Career's day" yaliyofanyika chuoni hapo alisema mikopo hiyo  inayotokana na 10% ya mapato ya halmashauri kama wataunda kikundi vyenye lengo la kufanikisha wazo fulani halmashauri wako tayari kuwashika mkono.

Mbali na hilo alisema hivi sasa jiji linauhitaji mkubwa wa watafiti na wabunifu kutoka kwenye idara ya teknolojia ya habari (Information technology IT) kwa lengo la kutatua changamoto mbalimbali pamoja na uboreshaji wa mifumo ya uendeshaji.

"Milango iko wazi kwa mwanafunzi yeyote akija na wazo hasa kwenye kutafuta majawabu ya changamoto tulizonazo, nitampeleka idara husika ili wazo lake liweze kufanyiwa kazi" alisema Dkt.Pima

Kwa upande wake Rais wa serikali ya wanafunzi Sunday Kathbet alisema siku hii inatoa fursa kwa wanachuo kuonyesha vipaji vyao lakini vitu wanavyovifanya wakiwa chuoni.

Siku ya vipaji na ubunifu chuoni hapo ilipambwa na mashindano kwenye kitengo cha biashara, teknolojia na vipaji ambapo walipata fursa ya kutumbuiza, kuwasilisha mawazo ya biashara na bunifu mbalimbali ikiwemo la kubadili makaratasi na maboksi yaliyotumika kuwa kadi.

Hata hivyo mgeni rasmi alipata fursa ya kutembelea maonyesho yaliyoandaliwa na wanachuo hao ambapo bidhaa za vyakula kama keki, nguo kama batiki na viburudisho ikiwemo sharubati na ubuyu vilivyotengenezwa na wanavyuo zilionyeshwa.

Mkurugenzi wa jiji la Arusha Dkt. John Pima akioneshwa moja ya kazi za sanaa ya uchoraji na mwanafunzi wa chuo cha uhasibu Arusha IAA Ines Shoo kwenye maonyesho yaliyoandaliwa na wanachuo siku ya kutambua vipaji na bunifu (Career's day) .

Mkurugenzi wa jiji la Arusha Dkt. John Pima akioneshwa ubuyu uliotengenezwa na mwanachuo wa chuo cha uhasibu Arusha IAA Lilian Ringo kwenye maonyesho yaliyoandaliwa na wanachuo siku ya kuonyesha vipaji na bunifu (Career's day)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...