Na Mwaandishi Wetu Mtwara

BODI ya wakurungezi ya Taasis ya Utafiti wa Kilimo nchini TARI) imepongeza watafiti wa kituo cha utafiti cha Naliendele TARI Naliendele) kwa kuwa na maendeleo ya kuridhisha na yanayoleta tija katika kubuni mbegu bora za mazao ya kilimo nchini.

Sambamba na hilo bodi hiyo imeitaka  kituo hicho waendelee kujitangaza zaidi ili wananchi haswa wakulima waweze kuwasikia na kupenda kutumia mbegu za mazao ambazo kituo hicho kinatafiti na kuzitoa kwa ajili ya kubadilisha na kuendeleza kilimo nchini.

“Rai yetu kwenu muongeze kujitangaza ili wananchi wengi haswa wakulima wawasikie na kupenda kuja kutumia mbegu, teknolojia na tafiti mbalimbali mnazozifanya kwenye kilimo,” alisema Mwenyekiti wa Bodi hiyo Dkt Yohana Budeba.

Wakati huo huo Dkt alitoa wito kwa halmashauri kutumia tafiti na tekinolojia za kilimo bora zinazobuniwa na watafiti wa taasisi hiyo  ili kuwasaidia wakulima kujikita katika kilimo bora na cha kisasa zaidi.

“Halmashauri zihimiwe kuunga juhudi zinazofanywa na Taasis yetu ya utafiti ambayo inafanya kazi kubwa na nzuri katika kutafiti na kubuni tecknolojia za kubadilisha kilimo chetu kuwa bora,” amesema.

Dkt Budeba amesema kuwa utafiti ni gharama kubwa na serikali imekuwa ikigharamia tafiti mbalimbali kupitia taasis hiyo ili kuboresha na kuendeleza kilimo cha kisasa kwa manufaa ya wakulima na  taifa kwa ujumla.

Amezitaka halmashauri ambazo hazijaanza kutumia tafiti  za taasis ya TARI katika kuelimisha wakulima wao kujikita kuanza kutoa nafasi kwa maafisa ugani na kilimo, kutoa na rasilimali fedha na watu waende TARI kujifunza na kuwasaidia wakulima katika maeneo yao kuendeleza kilimo.

Amesema kwa sasa ni Halmashauri 16 tu nchini ambazo zinaunga juhudi zinazofanywa na TARI nchini ambazo zinashirikiana na taasisi hiyo ya watafiti katika kuendeleza kilimo nchini.

“Halmashauri 16 zinajifunza na kutumia tafiti za taasisi yetu ya kilimo, tunaomba halmashauri zingine ziinge mfano wa hizo chache 16 ambazo zimewasaidia wakulima wao na sasa wanafanya kazi nzuri sana kwenye kuendeleza kilimo ,” amesema

Dkt Budeba ameongeza kuwa  60 ya mapato ya halmashauri nchini inatokana na kilimo hivyo ni bora halmashauri zikajikita zaidi katika kutumia utafiti na techknolojia ya kubadilisha kilimo ambayo inabuniwa na TARI.

Makamu Mwenyekiti wa Bodi hiyo Jacqueline Mkindi ameomba serikali kuendelea kuwekeza zaidi kwenye kuendeleza kuboresha mafunzo kwa watafiti ili waendelee kutoa huduma nzuri ya utaftiti nchini.

Amesema kilimo kinazidi kupanuka sana na kuwepo kazi kubwa ya kufanya tafiti zaid na hivyo kushauri serikali iendelee kuwajengea uwezo watafiti kwa kuwapa mafunzo zaidi ya utafiti.

“Pamoja na kwamba kuna fursa za masoko, mabadiliko ya tabia ya nchi, wadudu pamoja magonjwa ni baahdi ya matati ambayo yanazidi kuwepo kwenye kuendeleza kilimo hivyo ni vyema watafiti wetu wakaendelea kujengwa uwezo zaidi,” amesema.

Mtafiti wa zao la karanga kutoka kituo cha Utafiti cha Kilimo Naliendele akitoa maelezo kuhusu Kilimo cha karanga kwenye Shamba la mfano la Kituo hicho Naliendele

Wajumbe wa Bodi ya wakurungezi wa Taasis ya Kilimo Nchini (TARI) wakiwa katika Shamba la mfano la Kilimo cha karanga wakijifunza na kujionea mbegu Bora za karanga zinazotafitiwa na kubuniwa na kituo cha Utafiti cha Naliendele Mkoani Mtwara


Mkurungezi Mkuu wa Taasis ya Utafiti wa Kulimo Nchini (TARI) Dkt Geoffrey Mkamilo akisoma taarifa Kwa wajumbe wa Bodi ya wakurungezi wa Taasisi hiyo kuhusu shughuli za Utafiti zinazofanywa katika kituo cha Utafiti cha TARI Naliendele Mkoani Mtwara




Kaimu Mkurungezi wa Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Naliendele Mkoani Mtwara (TARI Naliendele) Dkt Fortunus Kapinga akitoa maelezo Kwa wajumbe wa Bodi ya Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Nchini (TARI) kuhusu ukuaji wa zao la korosho nchin. Wanaomsikiliza (Kutoka kushoto) ni Mwenyekiti wa Bodi hiyo Dkt Yohana Budeba (Wa pili kushoto) ni Mkurungezi Mkuu wa TARI Dkt Geoffrey Mkamilo. Wanaofutia ni wajumbe wengine wa Bodi hiyo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...