Na Chalila Kibuda,Michuzi TV

Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) imesema kuwa inaungana na Rais Samia Hassan Suluhu katika muongozo na maelezo aliyoyatoa katika hotuba ya April 6 mwaka huu yanayolenga kuboresha mazingira ya biashara na kuongeza ushiriki mpana wa shughuli za kujenga uchumi.

Akizungumza na waandishi wa Habari Mwenyekiti wa Sekta Binafsi nchini Angelina Ngalula amesema kuwa Sekta Binafsi inafarijika kumpata Rais anayeendelea kuamini Sekta Binafsi katika kukuza na kuinua uchumi wa maendeleo ya watanzania wote huku Rais akishauri na kuelekeza namna bora ya ukusanyaji wa mapato hivyo Sekta Binafsi itashirikiana na Serikali kuhakikisha wanasimamia misingi ya uzalendo na uadilifu katika suala zima la ulipaji kodi ili kazi iendelee kwa kasi zaidi.

Ngalula amesema TPSF inashauri mifumo ya kodi ifanyiwe marejeo na maboresho ili kuondoa migongano kati ya Taasisi zinazotoza Kodi na walipa kodi na tunaomba ushauri wa aliyekuwa Waziri wa Fedha na Mipango Dkt Philip Mpango ambaye ni Makamu wa Rais katika kikao cha Baraza la Biashara (TNBC) April 7 2019 aliongelea kuhusu uhitaji wa kufanya tathimini ya mifumo ya Kodi na kumnukuu"Mhe Rais nafikiri kwamba mifumo wetu wa kodi na umekuwa kukuu kama nakumbuka vizuri,mara ya mwisho kama taifa tumefanya a Comprehensive review ,ya mifumo wa kodi ,tozo, mapato yote ya Serikali na matumizi ilikuwa mwaka 2009 .Ninavyoona mimi Sasa , uchumi umebadilika na tunaendelea kutumia mfumo ambao ni out of date.Ndio maana malalamiko ni mengi Sana".mwisho wa kunukuu.

Aidha amesema katika eneo la ukusanyaji wa kodi wanashauri vitengo vya utafiti vya wizara Fedha na Mipango na Mamlaka ya Mapato Tanzania viimarishwe kwa kuwa na wataalam waliogombea katika masuala mbalimbali ya kitaalam kama kilimo ,Mafuta na Gesi,madini usafirishaji ,viwanda,Tehama,Ujenzi na Utalii na kipaumbele kitolewee kwenye matumizi ya Teknolojia ya Habari hasa matumizi ya Data katika kufanya uchambuzi wa data ili isaidie katika maamuzi mbalimbali.

Ngalula amesema katika kutanua uwigo wa walipakodi ni kurasimisha wafanyabiashara kwenye maeneo mbalimbali kwani zaidi ya asilimia 70 ya Sekta Binafsi siyo rasmi.

Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) Angelina Ngalula akizungumza na waandishi Habari namna walivyoipokea Hotuba ya Rais Samia Hassan Suluhu  katika kujenga mazingira ya biashara nchini.
Mkurugenzi Mtendaji wa TPSF Francis Nanai  akitoa maelezo kuhusiana na mkutano huo kwa serikali ya awamu ya sita .
Mkurugenzi wa Bodi ya TPSF Sylvester Koka akizungumza namna walivyojipanga.
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...