Na Jusline Marco,Arusha

Jaji Mkuu wa Tanzania ambaye pia ni mwenyekiti wa Tume ya utumishi wa mahakama Prof.Ibrahim Juma amesema tume hiyo itahakikisha inafanya shughuli za ujenzi wa miundombinu ya mahakama kwenye wilaya na mikoa ili wananchi waweze kufikiwa na huduma za kimahakama kwa urahisi.

Akizungumza jijini Arusha katika Mkutano uliofanyika kati ya Utumishi wa Mahakama na wajumbe wa Kamati za Maadili za Mkoa wa Arusha na Wilaya zake ambapo alisema  kuwa kama Tume huwa inapata nafasi ya kuboresha mpango mkakati wa kuboresha miundombinu.

Aidha alisema kuwa mpango mkakati uliopo sasa muda wake unakamilika mwaka huu ambapo wanapokwa maoni na mawazo kutoka kwa wadau kuhusu maeneo ambayo yana changamoto ya miundombinu ya majengo.

Vilevile alisema kuwa katika eneo la maadili Prof.Juma alisema kuwa kulingana na tathini iliyofanywa inaonyesha kuwa wananchi walio wengi hawafahamu vyema majukumu ya tume pamoja na kamati za maadili hali inayosababisha wao kuwasilisha malalamiko ambayo yanatakiwa kushughulikiwa kupitia mifumo ya kimahakama.

"Ninyi wajumbe mkiweza kufahamu mipaka ya kazi zenu mnakuwa na nafasi nzuri zaidi ya kuwaelimisha wananchi waelewe masuala ya nidhamu yakoje na masuala ya kimahakama yanakuwa ya aina gani."Alisema Prof.Juma

"Tumeshuhudia baadhi ya wananchi wakipeleka malalamiko kwenye mamlaka zisizo sahihi,masuala ya nidhamu wananchi wengi hawajui watakimbilia wapi,kwahiyo kazi ya tume ni kukutana na kamati zetu za wilaya na mikoa na kuwakumbusha vilevile kupekeka ujumbe kwa wananchi kwamba kuna njia ya kuwasilisha malalamiko dhidi ya vitendo vya ukiukwaji wa masuala ya nidhamu."Aliongeza Prof.Juma

Aliongeza kuwa kupitia muongozo mpya uliotungwa utawasaidia katika kufanya shughuli ya kuisaidia tume katika eneo la nidhamu ambapo alisema Tume ya Utumishi wa Mahakama imekuwa ikifanya ziara kwenye mikoa na wilaya na kukutana na wadau ambao wanahusika kwenye masuala ya utoaji wa haki.

Kwa upande wake Jaji Mfawidhi Mahakama Kanda ya Kigoma Mhe.Ilvin Mugeta alizitaka kamati za maadili za Mkoa na Wilaya  kutafakari na kuona namna ambavyo watafanya kazi kulingana na mazingira yaliyopo sasa hivi.

Aliongeza kuwa mfumo na muundo wa kamati za maadili uliopo kwasasa hauna tatizo lolote ambapo amewataka mahakimu wanaohusika na utoaji wa haki kutumika kwa umma na kufanya kazi zao kwa uwazi huku akieleza kuwa hakimu mfawidhi anayo nafasi ya kuishauri kamati katika utekelezaji wake wa majukumu.

"Hatutarajii mahakimu wanaoingia kwenye kamati kuacha kutekeleza majukumu yao vizuri ya kushauri kamati oli ziweze kutekeleza majukumu yao kwa nafasi zao kama wajumbe bila wivu,upendeleo,huba wala chuki kulingana na kiapo chao walichoapa."Alisisitiza Mhe.Mugeta

Awali akizungumza katika mkutano huo Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Ndg.Jerry Muro amesema kuwa moja ya changamoto ambazo hukutana nazo ni mabadiliko ya kiuongozi katika wilaya zao ambapo amewataka wajumbe wenzake kutumia muda kujifunza zaidi ili kuweza kuwahudumia wananchi jwa usahihi na haki.

Suzan Koila mjumbe kutoka katika Wilaya ya Ngorongoro ameeleza changamoto kubwa waliyonayo katika wilaya hiyo ni umbali wa mahakama moja kwenda mahakama nyingine ikiwa nibpamoja na uhaba wa mahakimu katika mahakama hizo ambapo ameomba tume hiyo kuwaongezea mahakimu ili kuweza kukidhi mahitaji kwa wananchi wao.

"Kutoka makao makuu ufike kata ya mwisho ni kilometa 398 sasa kwa mwananchi inakuwa ni vigumu kufika mahakamani akiwa na shida."alisisitiza Bi.Suzan

Akitoa neno la shukurani kwenye mkutano huo Mkuu wa Mooa wa Arusha,Iddy Hassan Kimanta ameiomba hazina ndogo kutenga fedha za uendeshaji wa vikao vya kamati ya mahakama na kuahidi kusimamia nidhamu na utendaji haki

Aliongeza kuwa katika masuala ya maadili kamati za wilaya na mkoa vinapaswa kujengewa uelewa wa kutosha ili mahakimu waweze kuwa na maadili ikiwa ni pamoja na jaji mfawidhi wa kanda ya Arusha kuanzisha programu ya kukutana na kamati hizo kila wilaya na kuzungumza nao na kuweza kuwajenga.

 Jaji Mkuu wa Tanzania ambaye pia ni mwenyekiti wa Tume ya utumishi wa mahakama Prof.Ibrahim Juma akizungumza na wajumbe wa kamati za maadili za wilaya na mkoa katika Mkutano wa Utumishi wa Mahakama na wajumbe wa Kamati za Maadili za Mkoa wa Arusha na Wilaya zake.

Mkuu wa Mkoa wa Arusha,Iddy Hassan Kimanta akitoa neno la shukurani katika mkutano huo uliofanyika jiji Arusha.

Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Ndg.Jerry Muro akieleza moja ya changamoto za mabadiliko ya kiuongozi katika wilaya ambazo hukutana nazo kwenye wilaya zao.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...