Hali
ya utapiamlo mkali kwa watoto katika halmashauri ya makambako mkoani
Njombe imetajwa kupungua baada ya serikali kuandaa mikakati mbali mbali
na kupambana na tatizo hilo.
Hayo
yamesemwa na Afisa Lishe wa Halmashauri ya mji wa Makambako SALMA
ABDALAH wakati akizungumza na waandishi ofisini kwake ambapo amesema
kuwa kwa sasa katika wodi ya kulaza watoto wenye Lishe duni hakuna
mgonjwa yoyote lakini wanaendelea na mpango wa kutoa elimu ya lishe kwa
wazazi ili kuendelea kupambana na tatizo hilo.
``kwa
sasa hali ya watoto wenye utapiamlo mkali imepungua kwa kiasi kikubwa
kwa sasabu kama unavyoona hapa wodini kwetu hakuna mteja hata mmoja
aliyelazwa kwenye wodi yetu na hii inapata kama wiki ya pili sasa,kitu
ambacho tunakifanya ni huduma tunazozitoa hapa kwa sababu tuna maziwa ya
dawa ambapo mtoto akija hapa anaanzishwa ``Amesema Bi Salma.
Veronika
Mutobe ni Muuguzi anayehudumia wodi ya watoto wenye lishe duni ambaye
amesema mara nyingi watoto wenye matatizo ya utapia mlo huathirika
kutokana na baadhi ya wazazi kutumia muda mwingi kufanya shughuli za
kibiashara na wakiwaacha watoto bila lishe bora Hivyo amewataka wazazi
kuhakikisha watoto wao wanawapa lishe bora.
``huu
ni mji wa kibiashara kinamama wengi baadhi yao hawazingatii maswala ya
lishe wakati fulani watoto wanaenda shule bila hata kupata chakuala,
mpango wetu ni kuendelea kuafikia kinamama kwenye maeneo yao ya kazi ili
kuwa elimu ya lishe``Amesema Mutobe
Aidha
Mutobe amekumbusha kuwa lishe ya mtoto inaanza tangu mtoto anapokuwa
tumboni hivyo amewataka Wazazi kufuata ushauri unaotolewa na wataalamu
wa afya kwa kuhudhuria klinik mapema na kula chakula bora.
Nao
baadhi ya kinamama mjini makambako wamekiri kupata elimu ya Lishe kila
wanapohudhuria kliniki na kuahidi kufanyia kazi ushauri wanaopewa na
wataalamu ili kuwakinga watoto wao na utapia mlo.
Mikakati mbalimbali imewekwa na halmashauri katika kuendelea kutoa elimu ya lishe kwa wanajamii.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...