Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Innocent Bashungwa ameipongeza Taasisi ya British Council kwa kuandaa warsha ya "Namna kijana anavyoweza kutumia ubunifu kujiendeleza kiuchumi".

 

Mhe.Bashungwa ametoa pongezi hizo Aprili 15, 2021 Jijini Dar es Salaam katika warsha iliyoandaliwa na Taasisi hiyo kuhusu  ushiriki wa wanawake kwenye masuala ya ubunifu (Woman in Creative Sector).

 

Hafla hiyo imeshirikisha wadau mbali mbali ikiwa ni pamoja na UNESCO na BASATA na   mada kadhaa kuwasilishwa ikiwemo   nafasi ya kijana kwenye ubunifu wa kujiendeleza kiuchumi.

 

"Nimefurahi kufika hapa, kwangu imekuwa ni fursa kubwa maana nimekutana na mwakilishi wa UNESCO, hivi karibuni nilikutana na Balozi wa AU tukafanya mazungumzo juu ya Mfuko wa Wasanii (Artists Trust Fund) ambao katika Bunge hili la Bajeti tumeazimia kuuanzisha na kunauhakika wa kupita kwa asilimia mia, sasa nikuombe kama itawezekana tupange wasaa mzuri ili tukutane na wadau tujue jinsi gani tunapanua Mfuko huu" amesema Mhe.Bashungwa.

 

Aidha, Mhe.Waziri ameshauri   Wadau wa Kimataifa wakiwemo UNESCO kuangalia namna wanavyoweza kutoa  mchango wao kusaidia kupanua Mfuko wa Utamaduni na Sanaa unaotarajia pia kuanza Mwaka ujao wa Fedha  wa 2020/2021.

 

Mhe. Bashungwa ametoa onyo kali kwa Wasanii wasiozingatia maadili ya kitanzania na kuwataka  kuwa na nidhamu ili kukubalika na hatimaye kuuza kazi zao.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...