NaJusline Marco-Arusha
Walimu wahitimu wa elimu maalum wametakiwa kuwa na moyo wa uzalendo kwa kujitolea katika shule mbalimbali nchini ambazo zinauhitaji wa wa taaluma yao ili waendelee kupata uzoezi na kuimarisha mafunzo ya ualimu waliyoyapata.
Akizungumza katika maafali ya 24 ya walimu elimu maalum yaliyofanyika katika chuo cha elimu maalum Patandi,Mkuu wa chuo hicho Lucian Erneo Segesela amesema kuwa kwa kufanya hivyo wataleta imani kwa serikali ili kutakapo tokea nafasi za ajira waweze kupewa kipaumbele.
“Niiombe serikali kuwapa kipaumbele walimu hawa ili wakazibe pengo la uchache wa walimu wa elimu maalum lakini pia niwaombe walimu hawa kuwa wakati wakiendelea kusubiri ajira wakaanze kujitolea kwenye shule mbalimbali zenye uhitaji ambapo hii itawafanya kusaidia jamii lakini pia kuongeza uzoefu,” Alisema Segesela.
Sambamba na hayo ameiomba serikali kupitia wizara ya elimu kutoa kipaumbele kwa walimu wahitimu wa elimu maalum ili waweze kuziba pengo la uhaba wa walimu wa elimu maalum katika shule mbalimbali nchini.
Aidha wahitimu wapatao 204 waliohitimu ualimu wa elimu maalum ngazi ya Stashahada na Astashahada katika chuo cha ualimu elimu maalum Patandi wameiomba serikali kutoa ajira kwa walimu tarajali ili kupunguza changamoto ya uhaba wa walimu hao mashuleni.
Kwa upande wake mgeni rasmi katika maafali hayo Emmanuel Kishosha ambaye pia ni meneja wa banki ya NMB Tawi la Clock Tower amesema kuwa pamoja na changamoto ta ukosefu wa ajira kwa walimu wa elimu maalum,kama wadau wanao fursa ya kuhakikisha wanasaidia chuo hicho katika kutatua changamoto mbalimbali.
Naye mmoja wa wahitimu hao aliyejitambulisha kwa jina la Fadhili Hashimu ameiomba serikali kuwapatia ajira walimu wa elimu maalum ambao wamehitimu masomo yao ili kuweza kuwasaidia watoto wenye changamoto mbalimbali katika kujifunza ikiwemo uziwi, uoni, usonji na ulemavu wa akili.
Sambamba na hayo katika risala ya wahitimu waliahinisha changamoto zingine ikiwemo serikali kutokuboresha maslahi yawalimu wa elimu maalum kwani wanapohitimu na kurudi vituoni hakuna motisha, uhaba wa vyumba vya madarasa, utoaji wa mafunzo ngazi ya cheti kwa walimu kazini ambao tayari wana vyeti pamoja na kutokamailika kwa jengo la utawala.
Muhitimu Fadhili Hashim akieleza changamoto zinazowakabili pindi wanapohiti masomo yao ya elimu maalum.
Wahitimu wa ualimu elimu maalum kwa fani za uoni,uziwi na ulemavu wa viungo wakifuatilia nasaha iliyokuwa ikitolewa na mgeni rasmi kwenye maafali yao ya 24 katika Chuo cha Ualimu Elimu Maalum Patandi Ndg Emmanueli Kishosha.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...