NA MWANDISHI WETU, MWANZA.
WAZIRI
wa Maji Jumaa Aweso amewataka mameneja wa Mamlaka za Maji nchini
kuwaeleza Mameneja Masoko wenu wasiwape wasoma mita malengo ya makubwa
ya makusanyo yasiyo halisia ambayo hayatekelezeki na yanawaumiza
wananchi na kusababisha malalamiko.
Badala yake aliwata mameneja
hao wasimamie kikamilifu zoezi la usomaji wa mita za maji ziwe halisia
ili kuepuka kuwabambikia wananchi bili za maji.
Aweso alisema
hayo leo wakati wa ziara yake mkoani Mwanza ambapo alisema ni haki ya
mwananchi kupatiwa huduma ya maji naye weajibu wake kulipa bili za maji
lakini zisiwe bambikizi kwao.
Aliyasema hayo wakati akiwa kwenye
mradi wa Maji wa Buswelo ambapo aliwaelekeza Mameneja Masoko hao
kuhakikisha wanasimamia kikamilifu suala za usomaji wa mita za maji ili
kuepusha malalamiko.
“Baadhi ya maeneo wananchi hulkalamikia
bili za pemaji naomnba wakurugenzi waelekezei mameneja masoko wenu
wasiwape malengo makubwa ya makusanyo wasoma mita yasiyohalisia maana
leo unampa malengo makubwa ya makusanyo hafikii atakachokifanya
atambamikizia bili mwananchi ili akuridhishe hivyo wekeni makarido
halisia”Alisema .
Hata hivyo aliwataka wahakikisha wanaweka
makadirio halisia juu ya kukusanya mapato ili wananchi waweze kulipa
bili stahiki ambazo sio kichefuchefu.
Katika hatua nyengine
amewataka Wakala wa Maji Vijijini Ruwasa na Mamlaka ya Maji ya Maji Safi
na Usafi wa Mazingira Mwanza kuhakikisha tenki lililopo eneo la Igogwe
na kahama tokea 2017 ambalo hakuna usambaji wowote wa huduma maji
wajipange miradi hiyo waende kuikamilisha na wananchi wapate huduma za
maji.
![]() |
WAZIRI wa Maji Jumaa Aweso akisistiza jambo wakati wa ziara hiyo kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongela |
![]() |
WAZIRI wa Maji Jumaa Aweso akisistiza jambo wakati wa ziara yake |
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...