BODI ya Wakurugenzi wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO)imesema shirika hilo limefanya kazi kubwa katika kuimarisha uzalishaji wa umeme Mkoa wa Mtwara na wanaotaka kuanzisha miradi au uwekezaji wowote wanaweza kufanya hivyo kwa kuwa kuna umeme wa kutosha.

Mwenyekiti wa bodi hiyo Dk.Alexander Kyaruzi amesema hayo wakati wa ziara ya wakurungezi wa bodi hiyo Mkoani hapa kwa ajili ya kujionea maendeleo ya miradi ya kuzalisha umeme katika Mikoa ya Mtwara na Lindi.

"Tumekuja Mtwara kujionea wenyewe kwa macho yanayojiri Mtwara, tuliambiwa kwamba uongozi wa shirika ulinunua machine mbili za megawati 4.3 kila moja na kituo cha kuzalisha umeme sasa kimeongeza megawati 8.6 za umeme zaidi," amesema.

Dk.Kyaruzi amesema hatua hiyo imesababisha kuongezeka kwa umeme kutoka megawati 18 ya umeme unaozalishwa katika kituo cha kufua umeme Mtwara mpaka kufikia megawati 30.4.Hatua hiyo ya kuongeza uzalishaji wa nishati ya umeme Mtwara umetokana na ukarabati wa mitambo ambayo ilikuwepo.

"Hali imewaftuliokuta hapa inafurasha, Mtwara kwa siku nyingi ilikuwa kama donda ndugu, baada ya kununua machine mpya mbili, umeme umetulia, tumefurahi sana kama bodi,"amesema.

Katika hatua nyingine, Dk.Kyaruzi amesema shirika hilo lipo mbioni kuanza ujenzi wa mtambo wa kufua umeme wenye magawati 300 mkoani hapa na hatua hiyo itasaidia kuongeza uzalishaji wa umeme Lindi na Mtwara.

Ameongeza mara baada ya kutembelea eneo la mradi katika Kata ya Naumbu Mtwara Vijijini, Dk.Kyaruzi amesema mategemeo ni makubwa kwenye mradi huo kuleta manufaa makubwa kwa wananchi wa Mtwara na Lindi. Umeme huo pia utapelekwa Dar es Salaam na mwingine utauzwa kwa nchi jirani ya Msumbiji.

Bodi hiyo pia imetembelea kituo cha kufua umeme Mtwara, kituo cha kupooza umeme Masasi na Lindi ambapo pia walijionea maendeleo na namna ambavyo vituo hivyo vinafanya kazi katika kusambaza umeme Lindi na Mtwara.

Wakurungezi wa Bodi ya TANESCO wakitembelea na kukagua mitambo ya kufua umeme katika kituo cha kuzalisha umeme Mtwara.Kituo cha kupooza umeme Wilayani MasasiMwenyekiti wa Bodi ya Wakurungezi ya Shirika la Umeme Nchini (TANESCO) (aliekunja mikono) pamoja na wakurungezi wengine wa Bodi hiyo wakiwa katika kituo cha kupooza umeme Masasi.
Wakurungezi wa Bodi ya TANESCO wakiwa katika eneo ambalo Shirika la Umeme linatarajia kujenga kituo cha kuzalisha umeme wa megawati 300 katika Kata ya Naumbu Mtwara Vijijini





Wakurugenzi wa Bodi wakiwa kwenye picha ya pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Danstan Kyobya baada ya kumfanya mkutano na waandishi wa habari kuhusu maswala ya umeme Wilayani humu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...