Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Chama hicho, Bi. Mercy Sila akizungumza na Waandishi wa Habari pamoja na Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Chama wakati akimpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan leo jijini Dar es Salaam.

Na Bakari Madjeshi, Michuzi TV

CHAMA cha Wafanyabiashara Wanawake nchini (TWCC) kimempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa utekelezaji mzuri wa majukumu yake tangu alipopata madaraka March, 2021 baada ya kufariki dunia mtangulizi wake, Hayati Dkt. John Pombe Magufuli.

Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Chama hicho, Bi. Mercy Sila amesema Chama cha Wanawake Wafanyabiashara kipo pamoja na Rais Samia katika kuhakikisha Tanzania ya sasa inafika malengo yake ya Uchumi wa Viwanda.

Bi. Sila amesema Chama hicho kinaamini yote yaliyoahidiwa na Rais huyo yatatekelezwa ipasavyo, amesema Wanawake Wafanyabiashara kwa sasa wana mazingira wezeshi, mazuri yanayowafanya wajione kama Wawekezaji nchini Tanzania.

“Sisi Wanawake Wafanyabiashara tunamaani malighafi zote zaidi ya asilimia 60 zinazotoka kwenye masuala ya Kilimo na biashara zenyewe ambazo zinazalishwa na Wanawake pia tunaamini zinachangia Uchumi wa Taifa letu la Tanzania”, amesema Bi. Sila. 

Kuhusu ziara ya Rais Samia nchini Kenya, Bi. Sila amesema anaamini Wanawake wa Tanzania na Kenya watafanya biashara kwa pamoja na wa Kenya hususan kwenye Biashara bila kujali Vibali vya Kazi na VISA kama iliyoelekezwa na Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta ili kuleta urahisi katika kufanya biashara hizo baina ya pande zote mbili.

“Tutashirikiana kwa pamoja kuleta maendeleo ya nchi zetu na maendeleo ya Jumuiya yetu ya Afrika Mashariki (EAC) katika masuala ya biashara na kuinua Uchumi kwa ujumla”, amesema Bi. Sila. 

“Ushindani wa Soko la Tanzania na Kenya, tunaamini Wanawake Wafanyabiashara wa Tanzania tumewazidi Wanawake wa Kenya, sisi tumeona kwenye maonesho ya Wanawake Wafanyabiashara, mambo makubwa yamefanyika, tazama Wanawake wa Kigoma kule tukishindana nao sisi wa Kenya hawatuwezi”, ameeleza Bi. Sila.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...