Charles James, Michuzi TV

MBUNGE wa Viti Maalum Mkoa wa Dodoma, Mariam Ditopile amewataka wananchi wa Jimbo la Buhigwe kutowachagua wagombea ubunge wa jimbo hilo kutoka upinzani na badala yake wampigie kura za kishindo mgombea wa Chama cha Mapinduzi CCM, Kavejuru Felix.

Ditopile ameyasema hayo leo kwenye mkutano wa kufunga kampeni za mgombea ubunge wa jimbo hilo la Buhigwe ambapo mgeni rasmi ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM na Makamu wa Rais, Dk Philip Mpango.

Amewataka wananchi wa Jimbo hilo kumchagua mgombea wa CCM, Kavejuru Felix kwani tayari anayo funguo ya maendeleo ambayo ni Ilani ya Uchaguzi ya CCM huku akisaidiwa na Makamu wa Rais, Dk Mpango na Rais Samia Suluhu Hassan.

“ Niwaombe sana ndugu zangu wa Buhigwe twendeni tukapime kura za shukrani kesho Mei 16 kwa Rais Samia, ambaye ametuheshimisha wananchi wa Buhigwe kwa kutupatia Makamu wa Rais wa Nchi, hii ni heshima kubwa kwenye Jimbo hili na Mkoa wa Kigoma.

Msimsikilize Zito Kabwe ambaye amejaa uongo, aliwadanganya kuwa atafunga kampeni leo kwa kutumia Helikopta lakini ameishia kutembea na gari, huyu ni mtu muongo asiye na aibu, kama amedanganya akiwa hawajashinda mkiwapa itakuaje? achaneni nao hawa wababaishaji wa siasa,” Amesema Ditopile.

Uchaguzi wa Buhigwe unafanyika kesho Mei 16 baada ya aliyekua Mbunge wake Dk Philip Mpango kuteuliwa kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Dodoma Mariam Ditopile akizungumza katika mkutano wa kufunga kampeni za mgombea ubunge wa Jimbo la Buhigwe kupitia CCM, Kavejuru Felix
Makamu wa Rais na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Dk Philip Mpango akisalimiana na wabunge ambao wameambatana nae katika kampeni za jimbo la Buhigwe mkoani Kigoma.
Wananchi mbalimbali waliojotokeza kwenye kampeni za mgombea ubunge wa Jimbo la Buhigwe mkoani Kigoma, Kavejuru Felix.
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...