NA YEREMIAS NGERANGERA…NAMTUMBO.
Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma imeuza kilo 529,758 za zao la ufuta kwa mfumo wa stakabadhi ghalani katika soko la kwanza katika chama cha ushirika NAPPACOS kwa msimu wa mwaka 2020/2021.
Mwenyekiti wa kamati ya stakabadhi ghalani ambaye pia ni afisa kilimo ,ushirika na umwagiliaji bwana joseph Mbilinyi alisema zaidi ya kilo 529,758 za ufuta zimeuzwa kwa mfumo wa stakabadhi ghalani kwa mnunuzi mmoja kampuni ya AFRISIAN GINNING LIMITED kushinda mnada huo kwa bei ya shilingi 2,282 kwa kilo..
Kwa mujibu wa mwenyekiti huyo alidai makampuni 7yalijitokeza kwenye mnada kutaka kununua ufuta huo kwa njia ya mnada ni Afrisian Ginning Limited shilingi 2,282, Hs implex limited shilingi 2,150,Sm Holding limited shilingi 2,221,Yihay Kerry limited shilingi 2,100.
Makampuni mengine ni RBST International limited shilingi 1,800 Mohamed enterprises Limited shilingi 2,150 na kampuni ya Export Trading Limited iliyopanga kununua ufuta huo kwa njia ya mnada kwa shilingi 2,024.
Mwajuma Ngonyani mwanachama wa chama cha msingi cha Mihagambo kilichopo katika kijiji cha Nangero pamoja na kuishukuru serikali kwa kuanzisha mfumo wa stakabadhi ghalani aliiomba serikali hiyo kuboresha maghala yaliyopo katika kata zao ili waweze kwenda kuhudhuria minada kutokana na hali ngumu ya kiuchumi waliyonayo wakulima wengi na kuamua bei ya mazao yao badala ya watu waliokuwa karibu na maghala au wenye uwezo wa kusafiri umbali mrefu ndio watakaoamua bei ya mazao yao..
Kupitia mnada huo vyama vya msingi vya ushirika vilivyopo katika wilaya ya Namtumbo vitapata kiasi cha shilingi 1,162,818,810 kupitia vyama vyao baada ya kutoa makato ya shilingi 87 kwa kilo kwa wakulima kadiri ya makubaliano ya kwenye kikao cha wadau wa stakabadhi ghalani kilichofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Namtumbo hivi karibuni.
Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo kwa mnada huo wa awali mzunguko wa fedha utakuwa wa shilingi 1,208,907,756 ikiwa malipo ya vyama vya msingi shilingi 1,162,818,810 huku ushuru wa Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo shilingi 30,196,202 na shilingi 14,833,224 kwa ajili ya mfuko wa maendeleo ambapo kwa sasa kila jumatano ya kila wiki kutakuwa na mnada wa zao hilo la ufuta.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...