Serikali
imeanzisha mipango wa kimkakati ya kukifanya Kiswahili kuwa bidhaa ya
Kimataifa ambapo tayari kuna wataalam wa Kiswahili wataalam 1318 ambao
wamesajaliwa na tayari vifaa vya kisasa vya mafunzo ya ukalimani kwa
vitendo na matumizi ya TEHAMA katika ukuzaji wa Kiswahili vimenunuliwa
na vimegharimu kiasi cha zaidi ya Sh. mil.181.
Naibu Waziri wa
Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Pauline Gekul amesema hayo leo
Bungeni Jijini Dodoma alipokuwa akijibu swali la Mheshimiwa Mussa
Ramadhani Sima Mbunge wa Singida-Mjini alilouliza Je? Serikali ina
mpango gani wa kuifanya Lugha ya Kiswahili kuwa bidhaa ya kimataifa ili
kuendeleza na kukuza utamaduni wetu duniani?
“Tayari tunao
mpango wa kufundisha Kiswahili kwa wageni kupitia Balozi zetu nje ya
nchi na Serikali imeboresha na kuimarisha mafunzo ya stadi za kufundisha
Kiswahili kwa wageni pamoja na kutoa machapisho ya Kiswahili Rahisi kwa
wataalam wetu” amesema Naibu Waziri Gekul.
Ameongeza kuwa
Serikali inaendelea kusaidia nchi zilizoonesha nia ya kuingiza Kiswahili
katika mitaala yao ya Elimu ikiwemo Afrika Kusini, Namibia, Rwanda na
Uganda.
Naibu Waziri amesisitiza kuwa mwaka 2019 wakati wa
Mkutano wa Wakuu wa nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa
Afrika (SADC), Serikali ilifanikiwa kukifanya Kiswahili kuwa moja ya
lugha nne rasmi zinazotumiwa wakati wa vikao na mikutano ya Jumuiya
hiyo.
Akijibu swali la nyongeza la Mhe. Sima kuhusu ongezeko la
msamiati wa Kiswahili, Naibu Waziri amesema Serikali kupitia Baraza la
Kiwahili la Taifa (BAKITA) imekuwa makini panapokuwa na mabadiliko
yeyote ya kimazingira, kieneo au matukio yoyote, BAKITA wamekuwa
wakitafuta misamiati mbalimbali na kuisanifisha misamiati hiyo.
Aidha,
Naibu Waziri ametoa rai kwa Watanzania kutumia lugha ya Kiswahili
ikizingatiwa dunia na nchi yetu mfano ugonjwa unaosababishwa na Virusi
vya Korona (COVID-19), BAKITA tayari wamesanifisha jina hilo na kwa
Kiswahili ugonjwa huo unaitwa UVIKO 19.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...