Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo inatarajia kuwakutanisha Maafisa Utamaduni na Michezo lengo ikiwa ni kujadili mikakati bora ya kuendeleza sekta hizo.

Akizungumza Mei 06,2021 katika mahojiano na Kituo cha Redio cha A FM Jijini Dodoma  Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo nchini, Yusufu Singo ameeleza kuwa kikao hicho kitakua cha siku mbili na kitaongozwa na mada mbalimbali pamoja na kujadili utekelezaji wa Sera,Kanuni na Miongozo mbalimbali ya Sekta hizo.

 Hata hivyo, Mkurugenzi huyo alitumia nafasi hiyo kueleza kuwa  maandalizi ya Mechi ya Simba na Yanga itakayochezwa Mei 08,2021 katika Uwanja wa Benjamin Mkapa yamekamilika.

“Habari na Michezo ni Sekta zinazotegemeana  sana  kwa  mfano mwisho wa juma hili  tuna mechi ya Simba na Yanga, bila  umma kuelezwa vizuri juu ya mechi hii inaweza kukosa msisimko” amesisitiza  Mkurugenzi Singo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...