JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limefanikiwa kuwaua majambazi watatu na kukamata silaha moja bastola aina ya REVOLVER.

Katika taarifa iliyotolewa na  Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, SACP Lazaro Mambosasa inasema kuwa Mnamo tarehe 11/05/2021 majira ya saa tatu usiku huko Mbagala jirani na ukumbi wa Dar Live majambazi wapatao watatu wakiwa kwenye Pikipiki namba MC 640 CGT aina ya TVS wakijiandaa kufanya ujambazi kwenye maduka na vibanda vya miamala ya fedha, lakini kabla hawajatimiza azma yao ya kufanya uhalifu.

Taarifa hiyo imesema Kikosi kazi cha kupambana na ujambazi cha Kanda Maalum Dar es Salaam kilipata taarifa na kujipanga vizuri, ambapo ilipofika majira saa nne usiku majambazi hao wakiwa kwenye pikipiki walipewa amri ya kusimama lakini walikaidi amri hiyo na kuanza kuwarushia askari risasi, ndipo askari wakajibu mashambulizi na kufanikiwa kuwapiga risasi sehemu mbalimbali za miili yao na kufariki dunia papo hapo.

"Kikosi hicho kilifanya ukaguzi kwenye eneo la tukio na kufanikiwa kupata silaha moja Bastola aina REVELVOR ikiwa na risasi tatu ndani ya magazine na walipopekuliwa kwenye miili yao walikutwa na risasi tano za bunduki ambayo haifahamiki ni ya aina gani." Imeeleza

JESHI LA POLISI KANDA MAALUM DSM KUIMARISHA USALAMA SIKUKUU YA EID EL-FITRI
Jeshi la Polisi Kanda Maalum kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama limejipanga kikamilifu kuimarisha usalama katika kipindi cha sikukuu ya Eid el-fitri inayotarajiwa kuadhimishwa tarehe 13/05/2021 au 14/05/2021 pindi itakapothibitishwa na Mh. Mufti wa Tanzania.

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam linawaasa wananchi wa Jiji la Dar es Salaam kusherehekea sikukuu ya Eid El-fitri kwa amani na utulivu na kujiepusha na vitendo vya uvunjifu wa sheria.

Jeshi la Polisi Kanda Maalum limejipanga kuimarisha doria maeneo yote muhimu zikiwemo nyumba za ibada, fukwe za bahari, kumbi za starehe na maeneo mengine yote yatakayokuwa na mikusanyiko mikubwa ya watu ili kuhakikisha Wananchi wote wanasherehekea sikukuu hiyo kwa amani na utulivu.

Pia wazazi wahakikishe watoto wao hawatembei peke yao bila ya kuwa na uangalizi wa karibu na kutowaruhusu kuogelea peke

yao, kitendo ambacho kinaweza kuzuia watoto hao kuzama kwenye maji.
Wamiliki wa kumbi za starehe wanatakiwa kufuata sheria, kanuni na taratibu za uendeshaji wa kumbi hizo.

Aidha, Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam limepiga marufuku Disko toto katika kumbi zote za starehe za hapa Jijini Dar es Salaam.

Vilevile Madereva wa vyombo vya moto wanatakiwa kuendelea
kufuata sheria za usalama barabarani ikiwa ni pamoja na kutoendesha magari au pikipiki wakiwa wametumia vilevi/pombe.

Hata hivyo Jeshi la polisi Kanda Maalum Dar es Salaam linawaomba Wananchi kuendelee kutoa ushirikiano kwa kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu kwa namba zifuatazo 0653616277, 0755980633 na 0769360416.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...