Na Mwandishi wetu, Kiteto
MBUNGE wa Jimbo la Kiteto Mkoani Manyara, wakili msomi mhe Edward Ole Lekaita, ametoa sadaka ya chakula kwa waumini wa dini ya kiislamu katika misikiti ya Kibaya kwa ajili ya kusherehekea sikukuu ya Eid el fitri.

Mjumbe wa Kamati ya siasa ya CCM Mkoa wa Manyara, Singo Ndoera amekabidhi vyakula hivyo kama sadaka iliyotolewa na Mbunge huyo kwa ajili ya waumini hao.

Singo amesema amemwakilisha mbunge huyo ambaye yupo jijini Dodoma kwa ajili ya kuzungumzia na kutafuta ufumbuzi wa changamoto mbalimbali za wananchi wa Jimbo la Kiteto kama walivyomtuma.

"Mheshimiwa mbunge yupo Dodoma ila nimemwakilisha na amesema yupo pamoja na ninyi ndiyo sababu akatoa hii sadaka ili kusherehekea sikukuu ya Idd," amesema Singo.

Amesema mbunge mhe Ole Lekaita ametuma salamu za Idd kwa kusisitiza suala la amani, upendo na ushirikiano kwa jamii zote ndani ya Jimbo la Kiteto.

Ameeleza kuwa mhe Ole Lekaita amesema wananchi wa Jimbo la Kiteto wanapaswa kuendelea kuwa kitu kimoja ili kuwaza maendeleo na kuwa na Kiteto mpya yenye neema tele.

Mwakilishi wa madhehebu ya Ansaar Muslim, Sheikh Ramadhani Bakari akipokea sadaka hiyo kwa niaba ya waumini wa miskiti ya Kibaya, amemshukuru mbunge mhe Ole Lekaita kwa kutoa sadaka hiyo.

Sheikh Bakari amesema sadaka hiyo itawanufaisha waumini hasa wasiokuwa na uwezo kwani imetolewa kwa wakati muafaka.

Amesema waumini hao wapo pamoja na Mbunge huyo na wanamuombea dua aendelee vyema na majukumu yake ya kuwawakilisha wananchi wa Jimbo la Kiteto.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...