Mfanyabiashara Ndama Hussein maarufu 
kama Ndama mtoto wa ngo'mbe katikati.

MFANYABIASHARA Ndama Hussein maarufu kama Ndama mtoto wa Ngo'mbe na Yusuph Hassan wanaokabiliwa na kesi ya Uhujumu Uchumi wameondoa nia yao ya kutaka kuingia makubaliano na DPP ili kumaliza kesi hiyo inayowakabili.

Aidha, washtakiwa hao wamewasilisha maombi katika Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam wakiomba mahakama hiyo iangalie uhalali wa hati ya mashtaka dhidi yao ya kujipatia USD 150,000 kwa njia ya udanganyifu.

Nia ya kujiondoa katika makubaliano na DPP, imewasilishwa leo Mei 11,2021 mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Godfrey Issaya na wakili wa utetezi wa washtakiwa hao, Peter Madeleka

Mapema Wakili wa Serikali Mwandamizi, Wankyo Saimon alidai mahakamani hapo kuwa upelelezi bado wa kesi hiyo bado haujakamilika.

Wakili Madeleka amesema wateja wake wanashangaa wanapoambiwa kuwa upelelezi wa shauri hilo bado haujakamilika wakati DPP alishapokea jarada la polisi na aliridhika kwamba upelelezi umekamilika ndipo akaleta kesi mahakamani.

Ameongeza kuwa, washtakiwa wanapaswa kuletwa mahakamani na si kusikilizwa kwenye CCTV kamera.

Hata hivyo, Wakili huyo alihoji kuwa ni sheria gani inayoruhusu kundelea na kesi bila washtakiwa kuletwa mahakamani?.

Akijibu hoja hizo, Wankyo amedai, Mahakama ya ya Hakimu Mkazi Kisutu haina malamlaka ya kusikiliza wala kutoa amri yoyote kwa kuwa kesi yao ni ya uhujumu uchumi itaendeshwa chini ya kibali cha DPP.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Mei 26, 2021 kwa ajili ya uamuzi

Washitakiwa hao wanadaiwa, kabla ya Januari 21, 2020 washitakiwa hao kwa udanganyifu, walighushi nyaraka/risiti ya kuhifadhi kwa lengo la kudanganya kuwa Kampuni ya Lockfort Security Company Limited imepokea kilo 100 za dhahabu kutoka kwa Samuel Kabula huku pia Machi 5, mwaka 2020 Mkoa wa Dar es Salaam, washitakiwa hao pia waligushi mkataba wa mauziano kati ya Cozac Logiatics International Company Limited ya Tanzania na Innovative Perspective Company Limited ya Botswana kwa lengo la kuonesha kuwa Kamapuni ya Cozac Logiatics International Company Limited imeingia mkataba wa kuuza dhahabu kilo 500 kwa kampuni ya Innovative Perspective Company (PTY) Limited kwa gharama ya dola 27,000 kwa kila kilo wakati si kweli

Ikaendelea kudaiwa kuwa, katika tarehe hizo Mkoa wa Dar es Salaam, washitakiwa hao waligushi nyaraka ya kuonesha kuwa Kamapuni ya Cozac Logiatics International Company Limited imeweka hati fungano ya kuuza kilo 450 ya dhahabu kwa kampuni ya Innovative Perspective Company (PTY) Limited wakati wakijua si kweli.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...