HALMASHAURI ya Wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma imeshindwa kuvuna ufuta kiasi cha ekari 5 na kuuacha ukaukie shambani kwa madai ya kukosa pesa kiasi cha shilingi milioni moja ya kuweka vibarua ili waweze kuvuna ufuta huo.
Kwa mujibu wa afisa kilimo wa halmashauri ya Wilaya hiyo bwana Laurance Ndaka pamoja na mkuu wa idara ya kilimo ushirika na umwagiliaji bwana Joseph Mbilinyi walidai idara iliomba fedha kwa mkurugenzi kiasi cha shilingi milioni moja ili kukamilisha zoezi la kuvuna na kujenga sehemu ya kuweka ufuta huo pamoja na kazi ya kupiga lakini toka mwezi wa nne waliomba kupewa fedha hiyo kwa mkurugenzi bila mafanikio walidai maafisa kilimo hao.
Idara ya kilimo katika halmashauri ya wilaya ya Namtumbo iliomba kupitia vikao halali vya kisheria vya Halmashauri kulima shamba la maonyesho kwa wakulima wa zao la ufuta ili wananchi waweze kujifunza kupitia shamba hilo la ekari tano.
Wazo hilo liliungwa mkono na vikao halali vya kisheria na awali halmashauri ilitoa shilingi milioni 2 kwa ajili ya kusafisha shamba, kulima pamoja na palizi hali iliyowafanya baadhi ya wakulima kuvutiwa kutembelea shamba hilo kujifunza.
Saidi kiokola na Sijawa Omari ni wakulima na vibarua waliowahi kufanya kazi katika shamba hilo wameshangazwa na hali ya shamba hilo kutovunwa na kuuacha ufuta ukikaukia shambani na kuikosesha halmashauri fedha nyingi ambazo zingepatikana kutokana na kuuza kwa ufuta huo kwa mfumo wa stakabadhi ghalani.
Kiokola alidai gharama iliyotumika kwa halmashauri ya milioni 2 na ile ya kuvunia shamba hilo ingerudi na kupata faida kubwa sana licha ya yeye kutokuwa mtaalamu ni kwa kuona hali ya uzalishaji ulivyo na kiasi cha pesa ambacho kingeweza kupatikana alisema kiokola.
Kutokana na kukauka kupita kiasi kwa ufuta huo wataalamu wanadai uvunaji wake unatakiwa ufanywe asubuhi na mapema na kwa kutumia maturubai wakati wa kuvuna kuepusha ufuta mwingi kudondokea ardhini.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...