Khadija Seif, Michuzi Tv
MISS Kilimanjaro mwaka 2019, Glory Letayo ameadhimisha Siku ya hedhi duniani kwa kugawa taulo (Pedi) kwa wanafunzi wa shule ya Sekondari Magadini iliyopo Siha Mkoani Kilimanjaro huku akiwataka warembo nchini kusaidia jamii inayowazunguka.
Letayo amesema harakati za kusaidia jamii sio jukumu la Serikali pekee bali ni suala la kila mmoja na hivyo amewaomba warembo wanaoshiriki Mashindano ya ulimbwende kwa sasa kukumbuka kusaidia jamii hasa Mabinti wadogo.
"Mojawapo ya Safari yangu ya Ulimbwende niliahidi kusaidia jamii hasa upande wa mabinti hivyo siku ya hedhi salama duniani inanipa fursa mimi kunikumbusha kuwa mabinti bado wanakabiliwa na changamoto ya kukosa Masomo kutokana na kukosa taulo za kujistiria," Amesema Letayo.
Hata hivyo Letayo amesema mbali ya kukosa taulo bado Mabinti wanakabiliwa na kukosa Elimu ya kujiamini pamoja na usafi pindi wawapo kwenye siku zao.
"Ni wakati wa mashirika na wadau wa elimu ya jinsia ,afya pamoja na taasisi mbalimbali kutoa ushirikiano kwa serikali katika kutoa elimu ya hedhi salama ili wanafunzi waweze kuhudhuria kwenye masomo yao kila siku na kuacha uoga na kuona hedhi kama ugonjwa wa kumfanya kukosa Masomo kila mwezi," Amesema Letayo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...