
Daktari wa hospitali ya Miracolo akichukua damu kutoka kwa Wananchi waliojitokeza kuchangia damu katika madhimisho ya miaka mitano ya hospitali ya Miracolo (PICHA NA HERI SHAABAN
Mmoja wa Wananchi akipima afya bure Segerea katika madhimisho ya miaka mitano ya hospitali ya miracolo (PICHA NA HERI SHAABAN)
Mmoja wa Wananchi akipima afya bure Segerea katika madhimisho ya miaka mitano ya hospitali ya miracolo (PICHA NA HERI SHAABAN)
Na Heri Shaaban
HOSPITALI ya MIRACOLO ya SEGEREA Wilayani Ilala wamewapima afya bure wananchi wa Segerea na maeneo ya jirani katika wiki ya maadhimisho ya miaka mitano ya hospitali hiyo.
Huduma hizo za matibabu bure wamezindua mwishoni mwa wiki ambapo mamia ya wananchi walijitokeza kwa wingi kupima afya zao.
Akizungumza katika uzinduzi huo Dkt.Bingwa wa Watoto wa Hospitali ya Miracolo Anna Deogratius alisema wiki moja ya madhimisho ya miaka mitano kutoa afya bure wamepunguza gharama za matibabu kwa wagonjwa.
"Hospitali yetu ya Miracolo imezindua upimaji wa afya bure segerea ambapo pia kuanzia juni Mosi hadi Juni saba wananchi watatibiwa kwa gharama za chini. "Alisema Dkt Anna
Alisema katika uzinduzi huo mamia ya wananchi wa Dar es Salaam na maneo ya jirani waliojotokeza kwa wingi katika kupewa huduma.
Alisema wananchi wengi wanaitaji huduma za afya lakini wengi wao wanakosa kutokana na Changamoto za maisha na ukosefu wa kipato.
Amewataka wananchi kujenga tabia za kupima afya zao kila wakati kwa ajili ya kujitambua.
Aidha Dkt,Anna alisema hutoaji huo wa huduma za afya bure kwa wananchi walipima magonjwa mbalimbali yakiwemo Kisukari, uzazi wa Mpango ,Upimaji wa damu salama,presha,Afya kinywa na meno,VVU,wingi wa damu na magonjwa nyemelezi.
Amewataka Wananchi kujenga Tabia ya kupima kila wakati sio kula dawa bila kupima magonjwa.
Kwa upande wake Afisa Tawala wa Hospitali ya Miracolo Jaqeen Sarakisa hospitali hiyo imeweka utaratibu wake endelevu itakuwa inawapima afya wananchi kila wakati.
Afisa Jaqreen alisema, Dhumuni la kutoa hiduma kwa jamii kuunga mkono juhudi za Serikali katika kusegeza sekta ya afya karibu na wananchi sambamba na kusaidia wananchi wasio na uwezo kupima afya.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...