RAWAN Dakik (20) yupo mbioni kuvunja rekodi ya kuwa mtanzania wa kwanza mwanamke na kijana mdogo zaidi barani Afrika kupanda mlima Everest ambao ni mrefu zaidi uliwenguni. Hadi sasa Rawan amefanikiwa kupanda mita 6,400 kwa siku nne pekee kutoka katika kambi maalumu ya mlima Everest ambayo ipo mita 5,300 kutoka usawa wa bahari.
Rawan ataanza mzunguko wa pili jumanne wiki ijayo ambapo atafikia mita 7,200 kwa siku tano.
Rawan ameeleza kuwa inachukua takribani miezi miwili kupanda mlima Everest ikiwa hali ya hewa inaruhusu kukwea mlima na kwamba amejipanga kumaliza kukwea mlima huo mrefu zaidi ulimwenguni wenye mita 8,850 kabla ya mwisho wa mwezi Mei.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...