Na.Vero Ignatus.
ASKARI wa Jumuiya ya Hifadhi za wanyamapori (WMA) wametakiwa kutumia ujuzi wa kisayansi na teknolojia walioupata, ili kufanya doria kwa kuzingatia na kuheshimu haki za binadamu pale wanapohisi kuna nyara za serikali.
Aidha wametakiwa kutumia njia nzuri za ukamataji na upekuzi, pale wanapohisi kuna eneo lina viashiria vya uwepo wa nyara za serikali.
Hayo yalisemwa jana na Mkurugenzi wa Jumuiko la Maliasili Tanzania (TNRF), Faustin Zacharia wakati wa kufunga mafunzo ya siku tatu, kwa askari 40 wa wanyamapori kutoka katika Jumuiya za Hifadhi za Wanyamapori za Enduiment na Lake Natron zilizopo wilayani Longido, yaliyofanyika Bomang’ombe Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro.
“Kweli malalamiko mengi kwa wananchi pale mnapohisi pana nyara za serikali mnaenda kuepkua watu bila kuzingatia haki za binadamu hili kaliangalieni sana katika utendaji wenu wa kazi,”alisisitiza.
Alisema tangu mwaka jana Jumuiko la Maliasili Tanzania kwa ufadhili wa Mfuko wa Wanyamapori Duniani (WWF), linatekeleza mradi wa BMZ wa mabadiliko ya tabia nchi, unaolenga kuondoa changamoto za mabadiliko hayo ili kuboresha uhifadhi wa wanyamapori Tanzania.
Mwakilishi wa Mfuko wa Wanyamapori Duniani (WWF) Prof. Noah Sitati alisema mradi huu umewezesha kuwarudisha vijana wa jumuiya walishindwa kuendelea kutokana na janga la Corona ambalo limeathiri dunia kwasasa,,hivi sasa wamewezeshwa kulipwa ili kuendelea na shuguli zao.
Mbali na utoaji wa mafunzo hayo, pia Jumuiko la TNRF limekabidhi vifaa vya kufanya tathimini na kukusanya takwimu za wanyamapori, katika Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori Enduiment, kwa ufadhili wa WWF.
Alisema vifaa hivyo ni simu janja za mkononi ,chaji ya mkononi (power bank), boksi la maoni, hadubini na kifaa kinachowezesha kupata mtandao (Reuters ).
“Vifaa hivi tumetoa kwa lengo la kuboresha utendaji wa kazi zenu katika maeneo mtakayoyafanyia kazi,”alisema.
Mwenyekiti wa kamati ya usimamizi wa mradi wa Hifadhi ya Wanyamapori Ziwa Natron, Lee Olduka alisema mradi huo umekuwa na manufaa makubwa kwa wananchi na wanyamapori pamoja na mifugo, kwa kupata bwawa kubwa la maji.
Alishukuru kwa mafunzo hayo na vifaa walivyopata kwani vitaboresha utendaji kazi wao na kutoa matokeo chanya.Meneja wa Hifadhi ya wanyamapori Enduiment Peter Milanga alishukuru kwa teknolojia mpya ya mawasiliano ambayo itawasaidia katika majukumu yao ya ukusanyaji wa taarifa, kwani awali walikuwa wakifanya kazi hiyo kwa kutumia karatasi.
Kwa upande wao askari wa wanyamapori Juliana Paskali kutoka Hifadhi ya Wanyamapori Enduiment na Ismail Jacobu kutoka ziwa Natron walisema mafunzo hayo yamekuja wakati muafaka, ambapo itawaletea tija na matokeo chanya kwani yatawawezesha kufanyakazi kwa ufanisi.
Akizungumza kwa niaba ya serikali Ofisa Wanyamapori wa Wilaya ya Longido Lomayani Saiguran alisema katika kulinda wanyamapori, rasilimali watu inahitajika hivyo uwepo wa askari wa Jumuiya za Wanyamapori waliowezeshwa wainaisaidia serikali kutoa huduma sehemu ambazo haiwezi kufika kwa wakati.
Askari
wa WMAS Kama wanavyoonekana katika gwaride wakati wa kufunga mafunzo ya
siku tatu, kwa askari 40 wa wanyamapori kutoka katika Jumuiya za
Hifadhi za Wanyamapori za Enduiment na Lake Natron zilizopo wilayani
Longido, yaliyofanyika Bomang’ombe Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro.
Mkurugenzi wa TNRF Faustine akiwa anafunga mazfunzo ya siku tatu kwa Askari wa WMA
Katika jambo ambalo halikutakiwa kabisa kufanya kiafya ni askari au mwanamichezo kuvaa barakoa. Tafadhalini acheni kuiga hovyo hovyo mambo.
ReplyDelete