Na Amiri Kilagalila,Njombe
Baada
ya kuchaguliwa kuwa mwenyekiti wa chama cha soka mkoa wa Njombe hapo
jana Thobias Lingalangala ameahidi kuanza mara moja ujenzi wa ofisi za
chama cha soka mkoa wa Njombe (Njorefa).
Ahadi
hiyo ameitoa baada ya kutangazwa kuwa mshindi wa nafasi hiyo kwa kupata
kura 18 na kumshinda mpinzani wake Yono Kevela aliyekuwa mwenyekiti wa
chama hicho ambaye alipata kura 0.
Alisema
yeye siyo mtu wa hadithi kwa kuwa hakuumbwa hivyo na kuahidi kuwa
mtekelezaji wa mambo na kumtaka katibu wake pia kuwa mtu wa vitendo
vinginevyo ajiuzulu mapema.
"Nataka
ofisi ya Njorefa ijengwe mara moja hii nimeagiza ifanyije tathmini leo
ili kesho nipewe ripoti na kesho kutwa ujenzi uanze" alisema
Lingalangala.
Alisema
kupata kura asilimia mia moja kutoka kwa wajumbe kwake ni deni kubwa
hivyo.licha ya uhenzi wa ofisi hiyo ana mpango wa kwenda kuvumbua vipaji
na kuvitambua vilabu vyote vya mkoa ili kuviwekea mazingira mazuri ya
ushiri katika ligi.
Akitangaza
matokeo hayo msimamizi wa uchaguzi Deogratiasi Mbisi alisema
Lingalangala amechaguliwa kwa kura zote za wajumbe walioshiriki uchaguzi
huo wapatao 18 pamoja na makamu wake Emmanuel Mbogela.
Pia
alimtangaza Obed Mwakasungula kuwa katibu mkuu ambaye pia alipata kura
18 huku mpinzani wake Abubakar Aziz ambaye hakuwepo kwenye uchaguzi huo
akipata kura sifuri.
Kwa
upande wa mwakilishi wa mkutano mkuu wagombea walikuwa watano ambapo
Evans Nyinge aliibuka kidedea kwa kupata jumla ya kura 11 na kuwabwaga
wapinzani wake.
Aidha Mbisi alimtangaza Lusubilo Mwakafuje kuwa mshindi katika nafasi ya kuwa mwakilishi wa vilabu.
Mara
baada ya kupatikana kwa uongozi huo wapenzi wa soka mkoani Njombe
akiwemo Solanus Mhagama na Judith Sanga waliishukuru kamati ya uchaguzi
pamoja na shirikisho la soka Tanzania TFF kwa kusimamia uchaguzi huo kwa
uliofuata taaratibu zote.
"
Tunamshukuru mungu kwani TFF kwa kushirikiana na kamati ya uchaguzi
pamoja na uongozi wa serikali kwa kuhakikisha uchaguzi unafanyika kwa
kufuata utaratibu uliowekwa" alisema Solanus.
Hata
hivyo Siku moja baada ya uchaguzi wa njorefa kufanyika ,kamati tendaji
ikiongozwa na mwenyekiti wa chama hicho Thobias Lingalangala imeunda
kamati mbalimbali ambazo zitasimamia maendeleo ya mpira mkoan humo na
kutoa onyo kwa ataezembea na kuonekana kikwazo katika jitihada za kukuza
soka
Akitoa ufafanuzi wa
kuharakisha uundwaji wa kamati na Aina ya Viongozi wasiotakiwa katika
kipindi hiki Cha kunusuru soka la Njombe ambalo linazidi kudidimia.
Lingalangala Amesema yeyote atakaeonesha kushindwa kuendana na Kasi yake
ajiengue kabla hajaenguliwa na Kisha kutoa agizo la uwajibikaji.
Kuhusu
kamati zilizoundwa na wajumbe wake, makamu mwenyekiti wa njorefa
amesema zipo 5 na kuwataja wajumbe wake pamoja Viongozi wa kamati hiyo
ambao papo hapo wameingia kazini.
Kamati
ambazo zimeundwa ni ni Kamati ya fedha ambayo mwenyekiti wake ni Erasto
Mpete ,Kamati ya Ligi na Mashindano ambaye mwenyekiti wake Lusubilo
Mwakafuje,Kamati ya Ufundi mwenyekiti akiwa ni Meshack Mnyawasa ,Huku
Kamati Vifaa mwenyekiti wake akiwa ni Musa Muhagama .
Kamati
zimeanza utekelezaji wa maagizo ikiwemo kuvitambua Tena vilabu vya ngaz
zote vya mkoa wa Njombe,maandalizi ya ujenzi w ofisi na kuirejeshea
makali Tena njombe mji ili kurejea kigi kuu misimu ijayo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...