Na Mwandishi Wetu,Michuzi TV

MKUU wa Jeshi la Polisi Tanzania IJP Simon Sirro leo Mei 31, 2021 amefanya mabadiliko madogo kwa Makamanda wa Polisi huku Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza Kamishna wa Polisi (ACP) Muliro Jumanne akihamishwa na kuwa Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam kuchukuwa nafasi iliyoachwa na Kamishna wa Polisi Camillius Wambura.

Mabadiliko hayo yanakuja baada ya Rais Samia Suluhu Hassan kumpandisha cheo Kamishna Msaidizi wa Polisi kuwa Kamishna wa Polisi na kumteua  kuwa Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) Camillus Wambura na Kamishna Msaidizi wa Polisi Hamad Khamis Hamad kuwa Kamishna wa Polisi na kumteua kuwa Kamishna wa Kamisheni ya Fedha na Logistiki.

Katika mabadiliko hayo madogo ndani ya Jeshi la Polisi, Mkuu wa Jeshi hilo IGP Simon sirro amesema leo Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) Lucas Mkondya amehamishwa kutoka kuwa Kaimu Kamishna wa Fedha na Logistiki Makao Makuu ya Polisi Dodoma  kuwa Mkuu wa Usalama Barabarani Tanzania.

Wakati Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rufiji Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Onesmo Lyanga amehamishwa kwenda kuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma kuchukua nafasi ya Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi Gilles Muroto ambaye anastaafu.

Aidha Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Ramadhan Ngh'anzi amehamishwa kutoka kuwa Boharia Mkuu kwenda kuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa  Mwanza.

Wengine walioguswa na mabadiliko hayo ni Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Mwamini Rwantale amehamishwa kutoka Kanda Maalum ya Dar es Salaam ambako alikuwa Mkuu wa Utawala na Menejimenti ya Raslimali watu kwenda kuwa Kamanda wa Polisi Kikosi cha Tazara.

IGP Sirro amesema Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza Kamishna wa Polisi (ACP) Muliro Jumanne  amehamishwa kwenda kuwa Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam kuchukuwa nafasi iliyoachwa na Kamishna wa Polisi Camillius Wambura.

Amesema Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Zuberi Chembera amehamishwa kutoka Makao Makuu ya Upelelezi Dodoma kwenda Makao Makuu ya Polisi Zanzibar kuwa Naibu Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa jinai Zanzibar ambapo wanachukuwa nafasi ya Kamishna wa Polisi Hamad Khamis Hamad.

Pia Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Stella Richard amehamishwa kutoka kuwa Kamanda wa Kikosi cha Polisi Tazara kwenda kuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...