Afisa Mwandamizi wa Miradi kutoka Benki ya Maendeleo TIB, Sonia Mlaki (kulia) akipokea zawadi ya mshindi wa kwanza kwa upande wa Taasisi za kifedha kutoka kwa Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Mh. Exahud Silaoneka Kigahe.

Benki ya Maendeleo TIB imeibuka mshindi wa kwanza kwa upande wa Taasisi za kifedha zinazoshiriki hayo Mkoani Tanga, ambayo yanafanyika katika viwanja vya Mwahako, Jijini Tanga.

Benki ya Maendeleo TIB imepewa tuzo hii kwa kuibuka kinara mwenye huduma na bidhaa zenye tija na manufaa kwa maendeleo ya nchi kwa ujumla tofauti na taasisi nyingine zilizoshiriki.

Zawadi hiyo ya ushindi wa kwanza ilitolewa Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Exahud Silaoneka Kigahe na ilipokelewa na Mwakilishi wa Benki ya Maendeleo TIB, Sonia Mlaki.

Wakati huo huo, Benki ya Maendeleo TIB imeibuka Mshindi wa Tatu kwenye Huduma za Bima zilizoko katika benki yaani ‘bancassurance’.

Maonesho ya Biashara Tanga yanaendelea mpaka tarehe 6 Juni, 2021.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...