Kufuatia uwepo wa ubovu wa baadhi ya Barabara Jijini Dar es salaam, Mkuu wa Mkoa huo Mhe. Abubakar Kunenge ameelekeza TARURA kuhakikisha inaanza Mara moja Ujenzi na ukarabati wa Barabara Muhimu zenye mashimo ili kuondoa kero na usumbufu kwa wananchi.

RC Kunenge ametoa agizo hilo wakati alipotembelea baadhi ya Barabara Jijini humo ambapo ameshuhudia uwepo wa mashimo yanayofanya vyombo vya usafiri kupita kwa tabu na kusababisha malalamiko kwa Wananchi Jambo lililopelekea kutoa agizo hilo.

Miongoni mwa Barabara alizotembelea RC Kunenge ni Vingunguti Darajani kuelekea Barakuda yenye urefu wa Km 1.24 ambayo kwa mujibu wa Mratibu wa TARURA Mkoa wa Dar es salaam Mhandisi Geofrey Mkinga amesema Mkandarasi amekabidhiwa Kazi leo na anatakiwa kukamilisha kazi kwa muda wa miezi miwili kuanzia leo ambapo Mkuu wa Mkoa ametaka Ujenzi kufanyika usiku na Mchana.

Aidha RC Kunenge ametembelea Barabara ya Gerezani - Machinga Complex yenye changamoto ya Mashimo ambapo amemuelekeza Meneja wa TARURA Jiji la Ilala Samwel Ndoven kuhakikisha ifikapo Jumatano ya Mei 19 Barabara ikamilike kwa ubora na kuanza kutumika.









 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Hivi mkuu wa mkoa anaelewa adha tunayopata barabara ya kimara mwisho kwenda Bonyokwa? Ni matope qakati wa mvua na makorongo kukiwa na jua,huku kuna wakazi wengi lkn barabara ni mbaya sanaa.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...