Mwenyekiti mpya wa UVCCM mkoa wa Iringa Anord Mvamba alisema kuwa ataendeleza maono ya mwenyekiti mstaafu ya kuhakikisha vijana wanakuwa na umoja na mshikamano.Mwenyekiti mpya wa UVCCM mkoa wa Iringa Anord Mvamba akipongezwa na viongozi mbalimbali mara baada ya kuibuka kuwa mshindi wa kuwa mwenyekiti mpya wa umoja huo.

Mjumbe wa umoja huoAizack Kikoti akipiga kura katika uchaguzi wa kumchagua mwenyekiti mpya wa umoja huo

Na Fredy Mgunda,Iringa.

UMOJA wa vijana wa chama cha mapinduzi mkoa wa Iringa umepata mwenyekiti mpya baada ya kufanya uchaguzi wa kuziba nafasi iliyokuwa imeachwa wazi na aliyekuwa mwenyekiti wa umoja huo Kenani Kihongosi kuteuliwa kuwa mkuu wa wilaya ya Arusha mkoa Arusha.

Katika uchaguzi uliofanyika katika ukumbi wa chuo cha chama cha mapinduzi (CCM) Ihemi uliopo wilaya ya Iringa,wajumbe wa baraza hilo walipigia jumla ya kura 183 na kuthibisha kuwa Anord Mvamba amechaguliwa kuwa mwenyekiti mpya wa jumuiya ya umoja wa chama cha mapinduzi mkoa wa Iringa.

Akitangaza matokeo ya uchaguzi wa kujaza nafasi ya mwenyekiti,msimamizi wa uchaguzi huo mjumbe wa halmashauri kuu ya taifa MNEC wa njombe Fidelis Lumato alimtangaza Anord  Mvamba kuwa ndio mwenyekiti mpya baada ya kupata jumla ya kura 181 za kutoka kwa wajumbe wote wa umoja huo.

Alisema kuwa jumla ya kura 329 zilipigwa na hakuna kura halali zilizoharibika hivyo mshindi wa kwanza Anord Mvamba alipata 181 na mshindi wa pili Fatma Rembo alipata 123 huku wa tatu Iazack Mgovano alipata kura 25

Alimalizia kwa kuwaomba vijana wote wa umoja huo kuvunja makundi yote waliyokuwa nayo na kuanza kufanya kazi kwa ushirikiano ili kuendelea kuijenga jjumuiya hiyo kuwa imara kama ilivyokuwa awali.

Baada ya ushindi huo mwenyekiti mpya wa UVCCM mkoa wa Iringa Anord Mvamba alisema kuwa ataendeleza maono ya mwenyekiti mstaafu ya kuhakikisha vijana wanakuwa na umoja na mshikamano.

Aliwataka vijana kuvunja makundi yote yaliyotokana na uchaguzi ili kuhakikisha wanakijenga chama na kutafuta fursa mbalimbali zitakazowainua kiuchumi.

Awali akitoa nasaa zake kwenye mkutano mkuu maalum wa uchaguzi wa kujaza nafasi ya mwenyekiti wa umoja wa vijana wa mkoa wa Iringa, uliofanyika katika chou cha Ihemi ,Mwenyekiti mstaafu wa UVCCM mkoani humo ambaye ni mkuu wa wilaya ya Arusha Kenani Kihongosi alisema kuwa ili kuwa na jumuiya ya vijana bora ambayo itapika vilivyo viongozi bora ni lazima kuhakikisha wanaendeleza ushirikiano ulikuwepo kwa viongozi wa chama na serikali.

Alisema kuwa kiogonzi wa umoja wa vijana akiendekeza Majungu, makundi na mpenda rushwa hawezi kuwa kiongozi bora kwenye kuimalisha umoja wa vijana ambao ndio tanuli la kuwapika viongozi bora.

Kihongosi aliongeza kwa kuwashauri viongozi wa umoja wa vijana mkoa wa Iringa kuendelea kuilinda ilani ya chama cha mapinduzi na katiba ya serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ili kudumusha umoja na amani ambao umedumu kwa miaka mingi.

Aliwaomba viongozi waliochaguliwa kuingoza jumuiya ya umoja wa vijana mkoa wa Iringa Uchaguzi usiwagawe bali ukawaunganisha upya kuwa na umoja utakaodumu kwa kipindi chote watakacho kuwa madarakani

Kwa upande wake kamisaa wa chama cha mapinuzi (CCM) wilaya ya Iringa ambaye pia ni mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela aliwataka vijana kutumia mitandao ya kijamii kujiongezea ufahamu badala ya kufanya mijadala ambayo huleta uchonganishi kwa taifa na jamii.

Alisema kijana mwenye maono huondoa uoga na katika kutafuta maendeleo na hutumia mitandao ya kijamii ili kujijengea uelewa wa kuchanganua masala mabalimbali ya maisha  pamoja na jamii inayomzunguka .

 

 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...