Na.Vero Ignatus Arusha
Mkuu wa mkoa wa Arusha John Mongela amehaidi uongozi shirikishi na kuwatumikia wananchi wa mkoa Arusha sawa sawa na kiapo chake alichokula.
Mongela ameyasema hayo wakati akizungumza katika hafla ya kumuaga aliyekuwa mkuu wa mkoa mstafu Idd kiamanta na kumkaribisha mkuu wa mkoa mpya hafla iliyofanyika katika ukumbi wa mkuu wa mkoa.
Amesema kuwa kwa kuwa Rais Samia ameweza kumwamwini na kumkabidhi mkoa wa Arusha anahidi uongozi shirikishi ikiwa Ni pamoja na kuwatumikia wananchi sawa sawa na alichokula kiapo.
Awali akitoa salamu pamoja na kuaga rasmi viongozi hao,Mkuu wa Mkoa mstaafu Idd Kimanta alimuomba Mkuu huyo kuhakikisha anakamilisha utekelezaji wa hospitali za Wilaya ya Longido,Ngorongoro pamoja na ujenzi wa Ofisi ya kisasa ya Jiji la Arusha.
Ameongeza kuwa Jiji la Arusha halina Ofisi ya mafaili ya Jiji yanatembezwa kutoka Jiji kupelekwa Njiro,kutoka Jiji kupelekwa Kilombero nilitamani kuona jengo kubwa jiji lenye hadhi ya Geneva of Afrika
Aidha Kimanta, alisema kuwa anamshukuru Mungu kwa kufikisha umri wa miaka 62 na kustafu salama ,kwani ametumika serikalini kwa miaka 39 ambapo amekuwa kiongozi wa kawaida kwa Mika 30 na kiongozi kwa Mika 9
Alisema kuwa Jambo ambalo atalikumbuka kwa wanaArusha zaidi Ni ni ushirikiano,upendo nilioupata kutoka kwa watendaji kazi wenzangu aliokua akitumika pamoja nao,ambapo amemuhakikishia Mongela anayechukua nafasi yake kuwa yupo mikono salama
''Kazi ya kuwatumikia wananchi siyo rahisi inahitaji kumtwnguliza Mungu,nilipokuwa nilipostaafu ndipo nilipojua kuwa nubeba mzigo mzito nilikuwa sikali kabisa lakini Sasa nalala,wengine wananioa pole Sasa mnanipa pole ya wakati mnatakiwa kunipongeza''alisema Kimanta.
Alisema watu wa Arusha wanabahati kwani amewakabidhi mtu ambaye anamfahamu kwa muda mrefu, ni familia,na pia ni mdogo wake ,Ila inapokuja kwenye masuala ya Uongozi yeye ni mkuu wa mkoa.




Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...