WASANII
wakongwe nchini Juma Kassim Kiroboto almaarufu kwa jina la Juma Nature
na Chegge Chigunda wameuzindua wimbo wao leo unaokwenda kwa jina la
'Kucha' kwa kupitia kipindi Cha Traffic Jam kinachorushwa na Redio
Clouds.
Wakizungumza
mara baada ya uzinduzi wa nyimbo hiyo ambao uko katika 'Audio' na
'Video' Nature na Chegge wamesema huo ni mwanzo wa kuleta mambo mazuri
kwa mashabiki wao ambao waliwakosa kwa kipindi kirefu.
"Ukituona
ni kama tunafanana lakini Jambo ninaloweza kusema ni kwamba sisi ni
wasanii wawili tofauti lakini tuna muunganiko mzuri kwenye ladha ya
uimbaji" alisema Nature.
Naye
Chegge amesema kuwa hivi sasa amerudi kivingine na pia yuko kwenye
usimamizi maalumu hivyo wote mmoja ana maneja wake ambao wanawasimamia
katika kazi zao.
Aidha
Mtangazaji wa kipindi Cha Traffic Jam Gadner Habash almaarufu kwa jina
la Captain alieleza umma ulikuwa katika uzinduzi huo uliofanyika katika
eneo la nje ofisini hapo kuwa wimbo huo umerekodiwa na mtayarishaji
mchanga mwenye maskani yake Mkoani Iringa aliyemtaja kwa jina la Halfan
Yahya almaarufu kwa jina la 'Tizo Touch'.
Kutoka
kushoto ni Mtangazaji wa Kipindi Cha Traffic Jum Gadner Habash
akifuatiwa na msanii Juma Nature, Mtangazaji wa Traffic Jam Fetty na
msanii Chegge Chigunda wakiwa katika picha ya pamoja mara baada uzinduzi
wa wimbo wa Kucha ulioimbwa na kurekodiwa kwa pamoja na wasanii hao
wakongwe ambao katika miaka ya nyuma walitamba na makundi ya TMK
Family na Wanaume Halisi.Msanii
wakongwe wa mziki wa Bongo Fleva Juma Kassim Kiroboto almaarufu kwa jina la Juma Nature akifafanua
jambo kwa waandishi wa habari hawapo pichani wakati wa uzinduzi wa
nyimbo wao leo unaokwenda kwa jina la 'Kucha' kupitia kipindi Cha
Traffic Jam kinachorushwa na Redio Clouds.
Wasanii wakongwe wa mziki wa Bongo Fleva Juma Nature na Chegge wakiingia katika Ofisi za Clouds Media wakati wa uzinduzi wa nyimbo wao leo unaokwenda kwa jina la 'Kucha'
Wasanii wakongwe wa mziki wa Bongo Fleva Juma Nature na Chegge wakiingia katika Ofisi za Clouds Media wakati wa uzinduzi wa nyimbo wao leo unaokwenda kwa jina la 'Kucha'
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...