Kampuni ya bima ya Sanlam imezindua kauli mbiu yake mpya iitwayo Ishi kwa kujiamini yaani Live with Confidence. 

 Akizungumza wakati wa uzinduzi huo Afisa Mtendaji Mkuu wa Sanlam Life Tanzania na Afrika Mashariki Julius Magabe alisema ‘’Leo ni siku ya muhimu sana kwa Sanlam, kwani tunakwenda kuzindua kauli mbiu na dhima yetu mpya isemayo “Live with Confidence” yani “Ishi kwa Kujiamini” Hii siyo kauli mbiu mpya tu ya Sanlam au maneno mafupi yanayokaa chini ya nishani ya kampuni yetu kama tu utamaduni.

Ndugu Magabe aliongeza kwa kusema ‘’hii ni ahadi yetu kwa wateja wetu na jamii nzima ya watanzania. Ni ahadi ya kufanya kila linalowezekana kwenye utoaaji wa huduma zetu, kumfanya mteja wetu kuishi kwa kujiamini akiwa na amani kuwa anayokinga madhubuti ya kifedha, dhidi ya madhara yanayotokana na majanga mbali mbali ya kimaisha, ama amani yakuwa bima yake ya akiba itaiva nakumwezesha kutimiza malengo yake.

Kampuni ya Bima ya Sanlam inatoa huduma kwenye Nchi Zaidi ya 34 Afrika na kwa hapa Tanzania, Sanlam inazo kampuni mbili za bima kwa maana Sanlam General Insurance (SGI) na Sanlam Life Insurance (SLI) . SGI ilianza biashara mwaka 1998 na SLI ilianza mwaka 2005, kwa pamoja, kampuni hizi mbili zinauzoefu wa kulihudumia soko la bima la Tanzania kwa miaka takriban 39.
 Afisa Mtendaji Mkuu wa Sanlam Life Tanzania na Afrika Mashariki Julius Magabe alisema akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...