Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ndugu Samia Suluhu Hassan amepokea kwa masikitiko, huzuni na majonzi taarifa ya kifo cha Mwanasiasa mkongwe na Kiongozi, Balozi  Abbas Kleist Sykes.

"Ni msiba mkubwa kumpoteza Kiongozi, ambaye licha ya kuwa kijana enzi za kuasisiwa na kuundwa kwa TANU, alishiriki, alishuhudia na aliunga mkono harakati za kupigania Uhuru wa Nchi yetu uliopatikana Disemba 9 mwaka 1961" - amesema Ndugu Samia Suluhu Hassan. 

Balozi Abbas aliyatumia maisha yake ya ujana katika kuijenga TANU, akiwa pamoja na Kaka zake Hayati Abdulwahid Sykes aliyewahi kuwa Rais wa TAA na Marehemu Ally Sykes aliyekuwa Mweka hazina wa Chama hicho.

Msingi uliowekwa na TAA mwaka 1929 ndio ulitumika kuanzisha TANU  Julai 7 mwaka 1954 chini ya uongozi wa Rais wa kwanza wa TANU Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na baadae kuungana na ASP ya Zanzibar kuunda CCM mnamo Februari 5 Mwaka 1977.

Balozi Abbas Sykes  ambae alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Kwanza  wa Dar es salaam, ametumikia Taifa akiwa Balozi katika Mataifa ya Canada, Ufaransa, Ubelgiji, Sudan Marekani, Mexico Hispania, Ureno, Morocco, Tunisia na Jamhuri ya Demokrasia ya Saharawi. Kazi aliyoifanya kwa uzalendo, uaminifu na uadilifu mkubwa. Pia, amekuwa Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa katika Shirika la Elimu na Utamaduni (UNESCO).

Chama Cha Mapinduzi kinatoa pole kwa familia ya Marehemu, Ndugu, Jamaa, Marafiki na Wananchi wote kwa msiba huu.

Mwenyezi Mungu mtukufu kwa uweza wake amlaze mahali pema peponi Balozi Abbas Kleist Sykes.
Hakika Sisi ni wa MwenyeziMungu na Kwake ni Marejeo Yetu.

Imetolewa na:

Shaka Hamdu Shaka
KATIBU WA HALMASHAURI KUU YA TAIFA
IDARA YA ITIKADI NA UENEZI
16 Mei 2021

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...