Na Yeremia Ngerangera, Namtumbo
VIONGOZI  wa serikali za vijiji 7 wakiwemo  wenyeviti wa vijiji ,watendaji wa vijiji ,wenyeviti wa kamati  ya maliasili wa vijiji  na waheshimiwa  madiwani  kutoka katika kata  za vijiji hivyo wamepatiwa mafunzo ya  utawala bora kutoka FORVAC  na MJUMITA.

Akifungua  mafunzo  hayo  mkuu wa wilaya ya Namtumbo  Sophia Mfaume  Kizigo aliishukuru FORVAC na MJUMITA kwa jitihada zao za kutoa elimu kwa jamii  kuhusu faida  ya kutunza  misitu  yao iliyopo  katika vijiji .

Kizigo  alisema mafunzo hayo yapate  wataalamu  wa uhifadhi  katika vijiji  watakaosimamia utawala bora ili lengo la uhifadhi  kwa jamii liongeze  faida  za kiuchumi,kijamii  na kimazingira  kutokana na usimamizi  endelevu wa misitu yao.

Hata  hivyo  kizigo aliwataka  viongozi  wanaopata mafunzo hayo  kuzingatia misingi ya utawala bora  ya  uwajibikaji,uwazi ,utawala wa sheria,maridhiano ,mwitiko,ushirikishwaji  na  kuleta ufanisi na tija katika jamii  wanayoiongoza.

Maulidi  Hamisi afisa misitu wilayani Namtumbo aliwaambia viongozi  wa vijiji  kuwa  viongozi  wa vijiji wengi  wanaohudhuria mafunzo ya misitu hawatoi  mrejesho  kwa wananchi  na badala yake  hubaki  nayo  wenyewe  hali  inayosababisha wananchi kutoelewa  dhana dhima ya uhifadhi wa misitu yao ya vijiji.

Hamisi aliwataka  viongozi  hao kwenda kutoa mrejesho  kwa wananchi katika vijiji  vyao ili wananchi waweze  kujua maana  na umuhimu wa uhifadhi wa misitu yao ya vijiji na kupunguza  migogoro  ambayo  inasababishwa  na kutotolewa  taarifa kwenye mikutano  ya maamuzi ya vijiji..

Naye Mwenyekiti wa  mtandao  wa jamii wa usimamizi wa misitu Tanzania  bwana  Revocatus  Njau  aliwataka viongozi hao wa  vijiji kuwa mfano wa kusimamia utawala bora katika uhifadhi wa misitu katika vijiji vyao .

Diwani wa kata ya Mkongo Daniel Nyambo  pamoja na kushukuru  FORVAC  na  MJUMITA kwa mafunzo ya utawala bora alieleza tatizo la uhifadhi katika vijiji vya Namtumbo kuwa  vijiji  vinaweza  kutenga maeneo ya hifadhi lakini wafugaji  wameenea katika maeneo yaliyotengwa na kuharibu maana ya uhifadhi .

Alisema  wakulima ni rahisi kuwaondoa lakini wafugaji  inahitajika nguvu za  ziada  za dola kuhakikisha  wafugaji  wanaheshimu  mipango ya vijiji  wanajifugia mifugo  katika maeneo ambayo hayastahili  kupelekwa  mifugo hiyo.

Mafunzo hayo  yalikuwa ya siku  moja yaliyofanyika katika ukumbi wa  Halmashauri ya wlaya  ya Namtumbo  na viongozi wa kijiji cha Kumbara,Limamu,kilangalanga,Chengena,Masuguru ,Njalamatata,Ligunga  pamoja na madiwani wa kata ya luchili,mchomoro,mkongo,mkongo gulioni  na limamu walihudhuria mafunzo hayo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...