Baadhi ya wanafunzi wa vyuo kutoka Jimbo la Kisesa wakiwa katika viwanja vya Bunge na Mbunge wa Kisesa, Mhe. Luhaga Mpina



Viongozi wa Umoja wa Wanafunzi wa Vyuo kutoka Jimbo la Kisesa wakiwa katika picha ya pamoja na Mbunge wa Jimbo la Kisesa, Mhe. Luhaga Mpina

Baadhi ya wanafunzi wa vyuo kutoka Jimbo la Kisesa wakiwa katika viwanja vya Bunge jijini Dodoma na Mbunge wa Kisesa, Mhe. Luhaga Mpina

Baadhi ya wanavyuo kutoka Jimbo la Kisesa wakiwa ndani ya ukumbi wa Bunge wakifuatilia Hotuba ya Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto



Sehemu ya baadhi ya wanavyuo kutoka Jimbo la Kisesa wakifuatilia mjadala wa hotuba ya Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto bungeni Dodoma.


Baadhi ya wanafunzi wa vyuo kutoka Jimbo la Kisesa wakiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Doroth Gwajima mara baada ya kuwasilisha hotuba yake bungeni Dodoma.


Umoja wa Wanafunzi wa Vyuo Vikuu mbalimbali nchini wanaotoka Jimbo la Kisesa wamefika bungeni kujifunza namna Bunge linavyoendesha shughuli zake huku wakiahidi kusoma kwa bidii ili waweze kutoa mchango unaostahili kwa jimbo lao na Taifa kwa ujumla.


Mwenyekiti wa Umoja wa wanafunzi wa vyuo kutoka Jimbo la Kisesa, Ndugu Sitta Kuzenza Nyangwakwa amesema umoja huo umeanzishwa kwa lengo la kuwakutanisha pamoja vijana wote wanaosoma vyuo mbalimbali kuanzia ngazi ya Diploma hadi Digrii wanaotoka Jimbo la KIsesa.


Amesema tayari wanafunzi wa vyuo wanaotoka Jimbo la Kisesa kutoka Mikoa ya Dodoma, Morogoro, Dar es Salaam, Mbeya wanaendelea kujiunga ili kuunga mkono juhudi za Serikali pamoja na Mbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina katika kuwaletea maendeleo ya jimbo hilo huku akitumia nafasi hiyo kuwahamasisha vijana wengine wanaotoka Jimbo la Kisesa kujiunga na umoja huo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...