Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Innocent Bashungwa akiwasilisha Hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Fedha ya Wizara hiyo kwa Mwaka 2021/2022, leo Mei 31, Bungeni Jijini Dodoma.
Na Eleuteri Mangi WHUSM, Dodoma
WIZARA ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo imevuka lengo la ukusanyaji mapato kwa kukusanya jumla ya kiasi cha Sh.1,
080,109,491 ambazo ni sawa na asilimia 113 hadi kufikia Mei, 2021 kutoka Sh.
960,000,000/= kiasi ambacho kilikadiriwa kukusanywa kwa mwaka 2020/21.
Hayo
yamesemwa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Innocent Bashungwa
alipowasilisha Bungeni Hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Fedha ya
Wizara hiyo kwa Mwaka 2021/2022.
Mafanikio
ya makusanyo hayo yanatokana na usimamizi wa makusanyo ya Serikali kwa
kuzingatia Sheria, Kanuni, Taratibu na Miongozo mbalimbali ya nchi na
kuongezeka kwa utoaji wa huduma zinazotolewa na Wizara katika sekta za Habari,
Utamaduni, Sanaa na Michezo.
Kuhusu
sekta ya Habari, Waziri Bashungwa amesema “Wigo wa vyombo vya habari umeendelea
kuongezwa nchini ili kuhakikisha wananchi wanapata haki yao ya kikatiba ya
kupata taarifa wakati wote kuhusu matukio mbalimbali muhimu kwa maisha na
shughuli zao”.
Hadi
kufikia mwezi Mei 2021 ina idadi ya magazeti na majarida yaliyosajiliwa 257;
vituo vya televisheni 43, vituo vya redio 200, televisheni mtandao 451, redio
mtandao 23, blogu 122 na jukwaa mtandaoni ni 09 hatua inayoonesha namna nchi
inavyoendelea kurahisisha na kuimarisha uhuru wa upatikanaji wa habari kwa
wananchi.
Katika
kuimarisha usikivu wa Redio za TBC,, Serikali imeendelea kuongeza usikivu wa
redio kutoka Wilaya 87 mwaka 2017 hadi Wilaya 102 mwaka 2021. Miradi
inayoendelea kutekelezwa kwa ajili
ya kuongeza mawanda na usikivu katika Wilaya za Ngara, Kyela, Ruangwa,
Kilombero na Ludewa ujenzi wa mitambo ya redio ya FM unaoendelea katika Wilaya
za Tanganyika, Makete, Uvinza, Mbinga na Ngorongoro itasaidia kuongezeka kwa usikivu a kufikia Wilaya 119 kati
ya Wilaya zote 161 sawa na asilimia 74 ambapo matarajio ya ni usikivu wa redio
kuzifikia Wilaya 134 sawa na asilimia 83 za Tanzania Bara pamoja na visiwa vya
unguja na Pemba kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022.
Katika
Sekta ya Utamaduni, Wizara imeanzisha Mfuko wa Utamaduni na Sanaa Tanzania
ambao ulisajiliwa Septemba 30, 2020 kwa lengo la kuwawezesha watendaji wa kazi
za kiutamaduni na kisanaa kimitaji na kuwajengea uwezo wa kitaalamu ili
kuwawezesha kuandaa bidhaa bora zinazomudu ushindani kitaifa na kimataifa.
Waziri
Bashungwa amesema matumizi ya Kiswahili yanaongezeka kwa kasi duniani na kuongeza kuwa kukubalika kwa lugha hiyo kunachagizwa
na msukumo wa kustawisha lugha hiyo unaoendelea kufanywa na unaoendelea
kufanywa na viongozi wa kitaifa akiwemo Rais wa Awamu ya Sita Mhe. Samia Suluhu
Hassan, aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tano Hayati Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na
watangulizi wao.
Waziri
Bashungwa amesisitiza kuwa Wizara yake iliendesha kongamano Mei 21, 2021 ambalo
lilizinduliwa na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa kwa lengo la
kutambua na kuenzi mchango wa Tanzania katika Harakati za Ukombozi wa nchi za
Afrika ili kutangaza, kuhamasisha, na kuelimisha jamii kuhusu urithi wa
ukombozi wa Bara la Afrika uliopo nchini.
“Mwaka
2011 Tanzania ilikabidhiwa na Umoja wa Afrika (AU) jukumu la kuratibu Programu
ya Afrika ya “Programu ya Urithi wa Ukombozi wa Bara la Afrika ambayo ilipewa
jukumu la kukusanya, kuhifadhi na kutangaza kumbukumbu kuhusu harakati za Ukombozi
wa Bara la Afrika ikiwemo nyaraka, makaburi, majengo, mahandaki, silaha, sare,
hotuba na magari kwa matumizi ya vizazi vya sasa na vijavyo ambayo makao yake makuu
yapo Jijini Dar es Salaam” amesema Mhe. Bashungwa.
Katika
sekta ya Maendeleo ya Sanaa, Wizara imefanikiwa kuendelea kuimarisha utoaji wa
huduma kwa wasanii na wadau wa sanaa ambapo Taasisi zinazowahudumia Wasanii za
BASATA, Bodi ya Filamu na COSOTA zimewekwa katika eneo moja kwenye jengo la
UTUMISHI lililopo Kivukoni. Hatua hii pamoja na mambo mengine, itawapunguzia
muda, kadhia na gharama wasanii wetu na wadau wengine wanaohudumiwa na Taasisi
hizi.
Waziri
Bashungwa amesema kuwa sekta ya Maendeleo ya Michezo nchini imeenedelea
kuimarika kwa timu na wachezaji mbalimbali kufanya vizuri katika mashindano ya ndani
na nje ya nchi.
Ameendelea
kusisitiza kuwa timu za mpira wa miguu nchini zinaendelea kufanya vizuri
ikiwemo Timu ya Tanzanite ya Wanawake wenye umri chini ya miaka 17 imefanikiwa
kutwaa Kombe la COSAFA baada ya kuzifunga timu kutoka Comoro, Afrika Kusini,
Zimbwabwe na Zambia nchini Afrika Kusini mwezi Novemba, 2020 wakati mchezo wa
ngumi mabondia Hassan Mwakinyo, Ibrahim Class, Salim Jengo, Tony Rashid, Bruno Tarimo
na Shabani Jongo wameendelea kupeperusha vema bdndera ya Taifa.
Wakichangia
hotuba hiyo, Wabunge Abbasi Tarimba, Seifu Gulamali na Nusrati Hanje wamesema sekta
za Sanaa na Michezo zinakukuza na kuongeza utalii nchini huku Mbunge Stanislaus
Nyongo akiwasisitiza Wabunge na Watanzania kumpigia kura Msanii Naseeb Abdul (Diamond
Platnumz) amabye ameteuliwa kuwania tuzo ya BET ya Best International Act.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...