Na Mwandishi Wetu, Michuzi TV.


MWENYEKITI wa Baraza la Makanisa ya Kipentecoste Tanzania (CPCT) Askofu Peter Konki amesema iwapo viongozi wa dini nchini watakutana na Rais Samia Suluhu Hassan miongoni mwa mambo ambayo watatamani kumwmabia kuhusu uchumi na hasa kuendelea kudhibiti mfumuko wa bei.

Akizungumza leo baada ya kufanyika kwa kikao cha viongozi wa dini, Askofu Konki amesema kuna mambo mawili iwapo watakutana na Rais watamwambia, kwanza muhimu ni eneo la  uchumi, kwenye uchumi ni vema Serikali ikaangalia mfumuko wa bei.

Amesema kwasababu walaji ni wale watu wa chini sana ambao uchumi wao haujakaa sawa , kupanda kwa vitu kuna watu wanaachwa hawana uwezo wa kununua vitu ambavyo vinaulazima kwao."Kwa mfano umeme umefika vijijini lakini kule kijijini kuna watu wengine wanaishi kwa kuuza mkaa , bado kuna watu wanafinyanga vyungu wapate mahitaji, bado kuna watu wanauza kuni waishi, kwahiyo utakuta hawawezi kununua umeme kwasababu umepanda haraka.

"Masikini na  matajiri wananunua umeme kwa bei sawa, hivyo Rais aangalie kwa jicho la tatu ili kumlinda mlaji wa mwisho ni la umuhimu sana.Vitu vyote ambavyo vitapandwa na watu wakaachwa nyuma bila kupata mahitaji yao Serikali iangalie kwa umakini,"amesema Askofu.

Aidha amesema umefika wakati kwa Serikali kuangalia namna ya kuwalinda viongozi walioko hai na waliotangulia mbele ya haki kwani kumekuwa na tabia ya kuwachafua na kuwasema vibaya viongozi hao na wanaofanywa hivyo wanaendelea kuachwa.

"Tunachoweza kusema sisi viongozi wa dini Serikali iwe inalinda viongozi wake wastaafu wawe waliondoka duniani au walioko hai, ni kukosa maadili kuwasema vibaya viongozi wetu.Kama mtu una mtoto wako na anaishi katika sio maadili na huna la kumfanya atasambaratisha familia. 

"Serikali iwe na sauti ya kutosha kwa wanaotoa  lugha chafu kwa viongozi.Kuna hili neno mwendazake, hili neno ni tusi , lakini kuna lawama nyingi juu ya Rais aliyeondoka, hawa watu tukiwanyamaziwa sio tu watasema kitu cha maana hata kwa Rais aliyeko madarakani."Sisi viongozi wa dini tunasema kwa ujumla wetu, viongozi wote waliondoka madarakani , hata waliotangulia mbele ya haki na hawa walioko ilimradi ameongoza nchi na atakeyeongozwa alindwe wakiwa madarakani na hata wakiwa nje ya madaraka,"amesema.

Ameongeza nafasi ya urais yoyote atakayepewa hawezi kuwa malaika , ataacha alama ya makosa na alama ya mazuri, hivyo kinachotakiwa ni kuchukua yale mazuri na mabaya aliyeko madarakani atarekebisa makosa, ndio maisha ya mwanadamu. 

"Lakini wakiachwa, leo mtu yuko hai anatoa mwingine mtu mwingine anasema kafa, kwanza hata mila zinakataa kabisa kumzushia mtu kifo, ukienda kule kwetu unaweza kutengwa na jamii mwaka mzima.Tunaomba Serikali wake ichukue hatua,  tusingependa kuona hayo yanatokea , kusikia lawama kwa Baba wa Taifa, mzee Mwinyi, Mzee Benjamin Mkapa ,ama kwa Mzee Kikwete au kwa Hayati Magufuli au kwa Mama Samia. 

"Maana kumtukana Mama ni kutukana Taifa la Tanzania , yuko madarakani unamtukana, yupo kwenye bendera unamtukana, yuko kwenye kila ofisi unamtukana basi tengenezeni lugha ambayo ina nguo, huwezi kumtukana baba yako au mama yako."Tunachafua taswira ya Taifa letu, niwaambie waandishi wa habari hili ni taifa lenu, taifa likiharibika hakuna pakwenda.Hata nyumbani baba ana mapungufu na yapo kila mahali,"amesisitiza Askofu Konki.

MWENYEKITI wa Baraza la Makanisa ya Kipentecoste Tanzania (CPCT) Askofu Peter Konki

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...