Na Mwandishi Wetu,Michuzi TV.
SHEIKH Mkuu wa Tanzania ,Muft Aboubakar Zubeir ametoa ombi kwa Serikali, Mahakama ,Ofisi ya DPP na vyombo vingine kuharakisha kusikiliza kesi na kutoa hukumu ya Waislamu waliopo kundi la Uamsho kwani wamekaa ndani muda mrefu.
Akizungumza leo Muft Zubeir amesema kwamba Waumini hao wa Dini ya Kiislamu ambao wanashikiliwa na vyombo vya ulinzi na usalama wamekaa muda mrefu na ni zaidi ya miaka tisa au miaka 10, hivyo ni vema Mamlaka husika zikaharakisha kesi yao, wale ambao watapatikana na hatia wafungwe, na watakaokuwa hawana hatia waachiwe.
"Kuna Waislamu wengi wametiwa ndani, wale wa Uamsho ni suala linaonesha wamekaa muda murefu kati ya miaka tisa hadi miaka 10, kama Muft niombe tu kwa mamlaka husika Mahakama , DPP na Mamlaka nyingine na Serikali kwa ujumla zile kesi zao ziharakishwe, watakaonekana na matatizo sheria ichukue mkondo wake na wale wataonekana hawana matatizo waachile.
"Kwani kukaa ndani muda mrefu halafu ukaonekana hauna tatizo nalo ni tatizo vile vile.Kwa hiyo hawa watu iangaliwe namna ya kumaliza kesi zao, zimechukua muda mrefu sana Mahakamani wanakwenda, wanarudi, wahukumiwe wale wenye kuhumiwa waende jela na wasio na hatia waachiwe,"amesema Muft Zubeir.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...