Na Amiri Kilagalila,Njombe
CHAMA cha Mapinduzi CCM mkoa wa Njombe kimewatahadharisha viongozi wa Chama hicho walioshindwa kufanya kazi kwa ufasaha kwa kipindi cha miaka 5 iliyopita ndani ya Chama katika uongozi wao na kuwataka kusahau nafasi hizo katika uchaguzi ujao wa mwaka 2022.

Hayo yamebainishwa na katibu wa Chama cha Mapinduzi mkoa wa Njombe Amina Imbo wakati akitoa salamu za Chama hicho katika baraza la jumuiya ya wazazi mkoa lililofanyika katika ukumbi wa ofisi za Chama hicho zilizopo Mji mwema halmashauri ya mji wa Njombe.

“Tunaelekea kwenye uchaguzi mwakani,kama kiongozi hujaweka alama katika eneo lako,haujafanya kazi kwa ufasaha katika jumuiya na Chama,ujue umejipoteza mwenyewe hatutaweza kukupa tena miaka miatano wakati tuliyokupa hukufanya chochote wala kubuni chochote,hiyo haikubaliki katika Chama cha Mpainduzi na Jumuiya zake”alisema Amina Imbo

Aidha ametoa wito kwa jumuiya ya wazazi kusimamia miradi ya maendeleo kikamilifu kwa kuwa jumuiya hiyo ndiyo iliyobeba jumuiya zingine katika Chama.

Kwa upande wake mwenyekiti wa Chama hicho mkoa wa Njombe Jassel Mwamwala katika salamu zake ametoa wito kwa viongozi na wanachama wa Chama hicho kuongeza kasi ya kutafuta wanachama wapya ili kuimarisha zaidi Chama hicho.

“Tumetangaza 1 mara 3 kwa kila mwanachama maana yake kila mwanachama kwenye jumuiya utuletee wanachama watatu ili Chama kiwe na Nguvu,huwezi kuwa na Chama kama huna wanachama.Na jambo jingine tunahitaji ada,ni lazima tulipe ada na viongozi tuwe wa mfano”alisema Mwamwala

Baadhi ya wajumbe wa katika baraza hilo akiwemo katibu wa jumuiya ya wazazi mkoa Bi, Agatha Lubuva na mwenyekiti wa Jumuiya ya wazazi wilaya ya Njombe Kasanga Makweta wamesema viongozi wataendelea kushiriakiana pamoja na kuhamasisha wanachama kulipa ada ya uanachama zoezi litakaloambatana na uuongezaji wanachama.
Katibu wa Chama cha Mapinduzi Amina Imbo akieleza mikakati ya Chama pamoja na kuwakumbusha viongozi wa Chama kutekeleza majukumu yao ili kujenga Chama pamoja na kuleta maendeleo kwa Jamii.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi mkoa wa Njombe Jassel Mwamwala katika baraza la wazazi mkoa wa Njombe akiwaomba viongozi kuwa na ushirikiano pamoja na kuongeza nguvu ya kupata wanachama.
Baadhi ya viongozi wa jumuiya ya wazazi wakiwa kwenye kikao cha baraza la wazazi wakiendelea kusikiliza na kujadili baadhi ya ajenda za baraza hilo ili kukuza jumuiya na maendeleo ya Chama.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...