Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe. Godwin Gondwe ameipongeza Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) kwa kuunda kamati za kushughulikia malalamiko wakati wa utekelezaji wa miradi ya Majisafi na Usafi wa Mazingira kuanzia ngazi ya Mtaa hadi Wilaya.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mafunzo na Mwongozo wa kushughulikia malalamiko hayo katika Wilaya ya Kinondoni ambapo ametoa maagizo kwa kamati hizo  kuleta mrejesho wa malalamiko yaliyopokelewa na  yaliyoshughulikiwa  kwa wakati ili ufanisi wa kamati hizo uonekane.

"Nimefurahi kuona DAWASA wamefika hadi  Kinondoni kutatua kero za wananchi kwa kasi, hivyo nipende kuzikumbusha hizi kamati za mitaa hadi wilaya zilizoundwa zikatimize majukumu yake kwa kutatua kero zitakazoibuliwa kwa wakati" alisema Mhe. Gondwe.

Akimkaribisha Mkuu wa Wilaya, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni Bibi Sipora Liana alisema kuwa utatuzi wa kero za wananchi katika kila sekta hususani wakati wa utekelezaji wa miradi ya Majisafi na Usafi wa Mazingira ni maelekezo kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ambaye ameagiza kero na malalamiko ya wananchi yasisubiri viongozi wa kitaifa zitatuliwe katika ngazi za chini. Bi Sipora pia ni Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya DAWASA

Akitoa shukrani kwa niaba ya Afisa Mtendaji Mkuu, Mhandisi Modester Mushi ambaye pia ni Mkuu wa Kitengo cha Mazingira ameishukuru Wilaya ya Kinondoni kupitia  Mkuu wa Wilaya kwa kutoa nafasi ya kuundwa kwa kamati hizo na kueleza kuwa mafunzo ya kusimamia malalamiko kwenye miradi ya majisafi imekwishafanyika katika wilaya za Ubungo, Ilala, Kigamboni, Kinondoni na Kibaha Mkoani Pwani.

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe. Godwin Gondwe

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...