KAMPUNI pendwa inayojali mahitaji na hali ya mwananchi wa kitanzania kwa muda mrefu sasa imekua ikitoa simu bomb ana za bei nafuu. Kwa miaka mingi sasa imekua ikiongoza kwa kuuza simu ambazo mtanzania wa hali yoyote ile anaweza kumudu kununua.

Sasa itel wameamua kuzidisha kusambaza upendo huo kwa kuwaletea wateja na wadau wake wa dhati bidhaa nyingine ili kufanya zoezi zima za kufurahia maisha liwe rahisi. Ukiachana na bidhaa nyingi ambazo itel wameleta, leo naomba nikufahamishe kwa ufupi kuhusu Laptop na TV za itel.

Zikiwa zimetengenezwa madhubuti kabisa kumlenga mtanzania, TV hizi za itel zimejaa rangi dhahiri, ambazo zipo vizuri kwa mng'aro. Mfumo wa TV ni wa kisasa uliowekwa ili kuonyesha maudhui ambayo macho ya mtazamaji yanatamani. Katika asili yake, huduma za televisheni dhamira yake ni kuwajulisha, kuelimisha, na kuburudisha. Kwa kulitambua hilo, bidhaa mpya za itel zinataka kufuata malengo hayo kwa kuwapa wateja vifaa bora vinayoenda na wakati.

Sambamba na TV, itel pia wameleta laptop kwa lengo la kuwafikia wanafunzi na watu ambao ni watumiaji wa kwanza wa laptop. Hii ilikua ni kwa ufupi tu, endelea kufuatilia kurasa zao za mitandao ya kijamii ili kujua zaidi kuhusu aina mbalimbali za TV pamoja na sifa za laptop yao.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...