Kama ilivyokawaida ya makampuni mengi husherehekea pale wanapomaliza jambo lao kwa mafanikio mwaishoni mwa wiki iliyopita TECNO walifanya hafla ya kusherehekea kwa kuhitimisha promosheni ya kwanza ya Camision Camping Kistaa na TECNO Camon 17 kwa mwaka huu wa 2021.

Shamrashamra za maadhimisho hayo zilisindikizwa na pongezi kwa washindi wa promosheni ya Camision Camping Kistaa na TECNO Camon 17 miongoni mwa washindi hao ni Patrick Alsina kijana mwenye kipaji cha kuimba ambacho bado hakijapata nafasi ya kusikika na wengi pamoja na Razack Mbaga kijana anayejishughulisha na upigaji picha walijishindia nafasi ya kwenda kutembelea Mbuga za Wanyama Mikumi wakiongozana na jopo la washindi wengine bila ya kumsahau Bwana Yusuph Yusuph Mjasiriamali anayejishughulisha na biashara ya utembezaji magazeti barabarani alijishindia Jokofu huku washindi wengine wakijishindia ving’amuzi vya DSTV na Drones.

Meneja Masoko TECNO akishindana kucheza na Angel Dansa maarufu wa lebo ya WCB.


Washindi wote waliopatikana kwenye promosheni hii walianza kwanza kwa kununua TECNO Camon 17 kabla ya kuingia kwenye droo kuu lililochezeshwa na msanii Elizabeth Michael siku mbili kabla ya hafla kubwa iliyofanyika Mbuga ya Wanyama Mikumi. TECNO Camon 17pro ni simu yenye kusifika kwa upigaji picha zenye rangi halisi kulingana na mazingira uliyopo simu hii inawezeshwa kufanya haya kupitia Kamera ya MP48 na kamera ya nyuma ya MP64.

Kampeni hii iliendeshwa na TECNO wakiwa kama wahusika wakubwa kwa kushirikiana na DSTV, Tigo kwa dhumuni la kuboresha na kupunguza gharama zinazotokana na upatikanaji wa habari kupitia mifumo ya kidigital Tigo imelisimamia hili kupitia ofa ya GB78 za internet zinazopatikana kwenye simu za TECNO Camon 17.

Sherehe hizo za maadhimisho zilipambwa pia na matukio mengine ikiwemo mashindano ya kuimba, kucheza, kuchekesha n.k vile vile wageni waalikwa ambao ni wasanii maarufu Jihan Mark na Idrissa Sultan walipata wasaa wa kupiga picha, kula pamoja na kujuana na mashabiki wa kazi zao za sanaa.

TECNO inawakaribisha katika maduka yote ya simu nchini Tanzania wakiendelea kutoa ofa mbalimbali pindi tu unuapo TECNO Camon 17pro.


Wakati wa kupata chakula cha mchana washindi wa Camission camping kistaa na Camon 17.


Sherehe hizo za maadhimisho zilipambwa pia na matukio mengine ikiwemo mashindano ya kuimba, kucheza, kuchekesha n.k vile vile wageni waalikwa ambao ni wasanii maarufu Jihan Mark na Idrissa Sultan walipata wasaa wa kupiga picha, kula pamoja na kujuana na mashabiki wa kazi zao za sanaa.

TECNO inawakaribisha katika maduka yote ya simu nchini Tanzania wakiendelea kutoa ofa mbalimbali pindi tu unuapo TECNO Camon 17pro.

Tembelea

www.tecno-mobile.com

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...