Na Leandra Gabriel, Michuzi TV
MAHAKAMA ya kikatiba nchini Afrika Kusini imemuhukumu aliyekuwa Rais wa nchi hiyo Jacob Zuma kwenda jela miezi 15 baada ya kukutwa na hatia ya kutoshiriki vikao vya kamati maalum inayochunguza tuhuma zake za ufisadi na kujihusisha na rushwa alipokuwa madarakani.
Hukumu hiyo imetolewa leo na jaji Khampepe Sisi ambaye amesema, hukumu hiyo haitakuwa ya lazima iwapo Jacob Zuma atazingatia na kuheshimu maagizo ya mahakama na kuanza kuhudhuria vikao vya kamati inayochunguza tuhuma za rushwa dhidi yake.
Awali Mwenyekiti wa kamati maalum inayochunguza tuhuma za Zuma, Raymond Zondo amekuwa akiiomba mahakama kumpeleke jela Zuma miaka miwili kwa kutoshiriki vikao vya kamati hiyo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...