Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango hii leo Juni 28, 2021 anaondoka nchini kuelekea Paris nchini Ufaransa  kumuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan katika Jukwaa la Kizazi Chenye Usawa ( Generation Equality Forum) litakalofanyika Paris Ufaransa kuanzia Juni 30 – Julai 2, 2021

 Jukwaa la Kizazi Chenye Usawa ( Generation Equality Forum) lina madhumuni ya kuchagiza usawa wa kijinsia kama yalivyokubaliwa katika mkutano wa Beijing uliofanyika mwaka 1995 baada ya kuonekana baadhi ya maadhimio yanasuasua.  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan aliridhia kuwa kiongozi katika eneo la haki za wanawake kiuchumi.

 Makamu wa Rais Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango ameongozana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki  Mhe.Balozi Mbarouk N Mbarouk, Katibu Mkuu Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto - Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii, Dkt John Jingu, Mkurugenzi wa masuala ya Jinsia na Watoto Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Bi. Nasima Haji Chum  pamoja na Kinara wa Uwezeshaji Kiuchumi  Mhe. Angela Kairuki

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...