Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Liberata Mulamula akipokea nakala ya hati za utambulisho kutoka kwa Konseli Mkuu wa Oman mwenye makazi Zanzibar Mhe. Said Salim Al Sinawi. Uwasilishwaji wa hati hizo umefanyika katika Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam



Konseli Mkuu wa Oman mwenye makazi Zanzibar Mhe. Said Salim Al Sinawi akizungumza na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Liberata Mulamula katika Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam mara baada ya kuwasilisha nakala ya hati za utambulisho



Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Liberata Mulamula akipokea nakala ya hati za utambulisho kutoka kwa Konseli Mkuu wa Msumbiji mwenye makazi Zanzibar Mhe. Agostinho Abacar Trinta katika Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam



Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Liberata Mulamula akizungumza na Konseli Mkuu wa Msumbiji mwenye makazi Zanzibar Mhe. Agostinho Abacar Trinta katika Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam mara baada ya kuwasilisha nakala ya hati za utambulisho

****************************

Na mwandishi wetu, Dar

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Liberata Mulamula apokea nakala ya hati za utambulisho za Makonseli Wakuu wawili kutoka Msumbiji na Oman wenye makazi Zanzibar.

Makonseli hao ni Mhe. Agustinho Abacar Trinta Konseli Mkuu wa Msumbiji pamoja na Mhe. Said Salim Al Sinawi Konseli Mkuu wa Oman

Pamoja na mambo mengine, viongozi hao wamedajiliana masuala mbalimbali ya kuimarisha uhusiano wa Kidiplomasia na Kiuchumi baina ya nchi zao na Tanzania.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...