Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. Hamad Hassan Chande (mwenye Kaunda suti) akioneshwa na Mkuu Wilaya ya Singida, Mhe. Paskas Mulagiri nyumba zilizozingirwa kwa maji zilizokuwa kando ya Maziwa Singidani, Kindai na Munang alipofanya ziara ya kikazi mkoani Singida



Mkuu Wilaya ya Singida, Mhe. Paskas Mulagiri akimuonesha Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. Hamad Hassan Chande na ujumbe wake athari za mafuriko kwa wakazi waishio kando ya Maziwa Singidani, Kindai na Munang alipofanya ziara ya kikazi mkoani Singida.


Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. Hamad Hassan Chande (wa pili kulia) akiwa katika ziara ya kukagua athari za mafuriko kwa wakazi waishio kando ya Maziwa Singidani, Kindai na Munang alipofanya ziara ya kikazi mkoani Singida.


Muonekano wa daraja lililobomoka kutokana na athari za mafuriko yaliyokumba wakazi waishio kando ya Maziwa Singidani, Kindai na Munang alipofanya ziara ya kikazi mkoani Singida.

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. Hamad Hassan Chande (wan ne kushoto) akiwa katika picha pamoja na Mkuu Wilaya ya Singida, Mhe. Paskas Mulagiri na maafisa mazingira kutoka mkoa wa Singida na wataalamu kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais mara baada ya kufanya ziara katika maziwa Singidani, Kindai na Munang.



Nyumba zikiwa zimezingiwa na maji ya maziwa Singidani, Kindai na Munang. Mjini Singida.

(PICHA NA OFISI YA MAKAMU WA RAIS)

………………………………………………………………………………….

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. Hamad Hassan Chande ameelekeza kukamilika haraka kwa mchakato wa kuyafanya maziwa wilayani Singida kuwa maeneo lindwa.

Chande ametoa maelekezo hayo kwa Mkuu wa Wilaya ya Singida, Mhe. Paskas Mulagiri alipofanya ziara ya kikazi katika maziwa ya Singidani, Kindai na Munang kukagua.

Alimuagiza Mkuu huyo wa wilaya pamoja na Manispaa ya Singida kusimamia kikamilifu mchakato huo kuweza kukamilika kwa wakati na kuandaa ripo ili Serikali itangaze rasmi maeneo hayo kuwa ni lindwa.

Aidha, Naibu Waziri huyo aliwatahadharisha wananchi waishio katika maeneo hayo kuacha kufanya shughuli za kibinadamu kando ya maziwa ili kuepuka madhara zaidi yanayoweza kutokea.

Katika hatua nyingine Chande alielekeza uongozi wa wilaya na manispaa hiyo kuwa na utaratibu wa kutenga maeneo salama kwa ajili ya makazi ya wananachi waishio kando ya maziwa.

Kwa upande wake Mkuu Wilaya, Mulagiri alisema kuwa mchakato wa kuyafanya maziwa hayo kutambulika kama maeneo lindwa unaendelea vizuri.

Alisema utambuzi wa mipaka unafanyika na utakamilika ndani ya kipindi cha muda mfupi ujao ili Serikali iweze kutangaza kuwa hayo ni maeneo ya hifadhi na kuwa na nguvu ya kisheria kuyasimamia.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...