RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi. Dk. Hussein Ali Mwinyi leo amemuapisha Mwenyekiti wa Tume ya Maadili ya Viongozi wa Umma Assa Ahmad Rashid pamoja na Abdalla Mzee Abdalla ambaye amemuapisha kuwa Kamishna wa Kamisheni ya Utumishi wa Umma.

Hafla ya kuapishwa viongozi hao ilifanyika Ikulu Jijini  Zanzibar ambayo ilihudhuriwa na viongozi mbali mbali wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar akiwemo Makamo wa Kwanza wa Rais Othman Masoud Othman, Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Hemed Suleiman Abdulla, Jaji Mkuu wa Zanzibar Omar Othman Makungu, Spika wa Baraza la Wawakilishi Zubeir Ali Maulid, Mawaziri na Mwanasheria Mkuu wa Serikali Dk. Mwinyi Talib Haji.  

Wengine ni Katibu Mkuu Kiongozi na Katibu wa Baraza la Mapinduzi Mhandisi Zena Ahmed Said, Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Idrissa Kitwana Mustafa, Makatibu Wakuu, Viongozi wa dini, Wakuu wa Vikosi vya Ulinzi na Usalama, viongozi wengine wa Serikali pamoja na Wanafamilia.


 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...