Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla amewaelekeza Mkuu wa Wilaya ya Ilala na Mkurugenzi wa Jiji la Dar es salaam kuja na Mpango Mkakati wa Kuendeleza na Soko la Machinga Complex ili Soko hilo liwe kimbilio kwa Wamachinga na Wateja.

RC Makalla ametoa maelekezo hayo alipotembelea Soko hilo na kusikiliza kero za Wafanyabiashara sokoni hapo ambao wamemueleza sababu zinazopelekea Wafanyabiashara kulikimbia Soko hilo na kwenda mitaani.

Miongoni mwa Kero zilizotolewa na Wafanyabiashara hao ni mazingira mabovu ya kufanya biashara,   Utaratibu mbovu wa kupata vizimba, Kodi kubwa, Sheria kandamizi,  Ushirikiano mbovu wa Viongozi, Umeme, Maji, Vyoo, Maji taka, Miundombinu isiyorafiki na utaratibu wa kulipa Kodi ya mwezi badala ya Ushuru wa siku.

Kutokana na Malalamiko hayo RC Makalla amewaelekeza Mkuu wa Wilaya na Mkurugenzi wa Jiji kuhitisha vikao vya Mara kwa Mara na Wafanyabiashara hao na kupeana Mrejesho wa utatuzi wa kero zao ili mwisho wa siku biashara zifanyike na Serikali ipate Mapato.

Aidha RC Makalla ameelekeza Viongozi wa Soko hilo kuachana na tabia ya kufungia biashara za wapangaji wanaoshindwa kulipa Kodi na badala yake wakae mezani kuangalia namna Bora.

Pamoja na hayo RC Makalla ameelekeza Halmashauri ya Jiji kufuatilia fedha za NSSF zilizotolewa Kama mkopo wa Ujenzi wa jengo hilo lili kujua Kama mkopo umemalizika au bado Deni lipo.






 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...